MISOKOTO YA BANGI YAMPELEKA WEMA SEPETU MAHAKAMA YA KISUTU, AKAA MAHABUSU SIKU SITA
Msanii Wema Sepetu.
Dar es Salaam. Msanii maarufu wa filamu, Wema Sepetu (28) na wengine wawili akiwamo mfanyakazi wake wa ndani, wameachiwa kwa dhamana kutokana na mashataka ya kukutwa na bangi.
Wema na wenzake hao wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota mahabusu kwa takriban siku sita.
Mfanyakazi wa msanii huyo, Angelina Msigwa (21) pamoja na Matrida Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima wamesomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga.
Msanii Wema Sepetu akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Akimsomea mashtaka hayo, Wakili Katuga alidai kuwa Wema ambaye ni mshindi wa taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikutwa na msokoto mmoja na vipande viwili vya bangi hiyo Februari 4, mwaka huu, nyumbani kwake Kunduchi Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam
Washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na Wakili Katuga aliieleza Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo amewaachia washtakiwa hao kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kusaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni kila mmoja. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 22, itakapotajwa tena.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment