BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDAMA WA NG'OMBE WANYESHWA UJI KUFUATIA UKAME KUIKUMBA MVOMERO MOROGORO.




Juma Mtanda, Morogoro
Ng’ombe zaidi ya 2,700 wameripotowa kufa kwa njaa katika kitongoji cha Ranchi-Sokoine Wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro huku ng'ombe na ndama wakinyweshwa uji na pumba za mahindi ili kunusuru uhai wao.

Wakizungumza na MTANDA BLOG katika mahojiano maalumu baadhi ya wafugaji wa kitongoji hicho walisema, majani yamekauka katika eneo halo na hakuna maji hali inayosababisha mifugo yao kufa kila siku.

Safina Payo ni mmoja wa wafugaji eneo hilo anasema; “Tunalazimika kuwanyweshwa uji ndama kutokana na mama zao kufa baada ya kuzaa na ngombe wengine tunawapa pumba ili kuwasaidia waweze kuishi”alisema Payo.

Safina alisema katika kitongoji chao kuna ukame ambao haujawahi kutokea na kwamba hata ikitokea ng’ombe jike akajifungua hana uwezo wa kutoa maziwa na badala yake yanatoka mapovu.

“Maji safi hakuna na maji yaliyopo yanachumvi nyingi hata sisi tukinywa huwa matumbo yanatuuma na mifugo wakinywa inawaathiri kwenye utumbo yao pia”alisema.

Hata hivyo mfugaji mwingine, Christina Kibonda alisema kuwa eneo lao limekumbwa na ukame tangu kiangazi cha mwaka jana 2016 na kuanzia kipindi hicho mpaka sasa mifugo bado inaendelea kufa.
Ni kweli tunawanyweshwa uji hasa ndama maana mama zao wanakufa mara baada ya kuwazaa na hata wasipokufa hawana maziwa”alisema.

Alisema kuwa wengi wa wafugaji wanchokifanya kwa sasa ni kununua majani na pumba yanayouzwa kwa ghalama kiasi cha Sh100,000 na kwamba kutokana na ukame huo ng’ombe wao wamekonda hivyo bei ya ng’ombe imeshuka thamani.

“Mwanzo wa ukame wakati unaanza mfugaji alikuwa na uwezo wa kutumia kiasi cha sh100,000 na zaidi kununua pumba na majani mabichi lakini siku zilipokuwa zinaendelea chakula kilikuwa hakitosherezi kwa mahitaji ya mifugo kulingana na uwingi wake.”alisema Christina.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Sokoine- Ranchi kijiji cha Wami-Sokoine, Maiko Mgema alisema kuwa mpaka sasa ni mifugo 2700 tayari wamekufa na wanaendelea kufa kutokana na ukame huo katika kitongoji hicho pekee.

Mgema alisema kuwa wafugaji wengi wamepoteza mifugo kutokana na kufa na imefikia hatua baadhi ya wafugaji kuwanywesha uji ndama ili kuwanusuru na kifo lakini jambo hilo limekuwa halisaidii na baada ya siku chache ndama hao hufa.

“Unajua panapotokea janga kila mtu anatumia kila aina ya mbinu kunusuru jambo na baada ya ukame kutokea na mifugo kufa baadhi ya wafugaji kumekuwa wakiwanywesha uji ndama ili wasife kutokana na mama zao kushindwa kutoa maziwa kwa sababu ya lishe duni.”alisema Mgema.

“Wenyeji wetu wanaotuzunguka katika maboma ya wafugaji wamekula nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo mpaka wamekinai nyama na imefikia hatua wanyama hao wanakufa hakuna anayewajali tena.”alisema Mgema.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Mohamed Utalii alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya athari zinazotokana na ukame katika wilaya hiyo, alisema kuwa suala hilo kwa sasa lipo mikono mwa rais John Magufuli.

Utalii alisema kuwa suala la ukame na baa la njaa lipo mikononi mwa rais yeye ndiye anayepaswa kutoa ufafanuzi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: