BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ULINZI MKALI HOSPITALI ULIPOHIFADHIWA MWILI WA NDUGU RAIS WA KOREA KASKAZINI

Maafisa wa serikali ya Malaysia wamesema bado hawajabaini nini kilisababisha kifo cha ndugu wa rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Mkurugenzi mkuu wa afya Noor Hisham Abdullah amewaambia wanahabari kwamba hawajapata ushahidi wowote wa kutokea kwa mshtuko wa moyo au vidonda vilivyotokana na kudungwa mwilini.

Amesema uchunguzi kwenye maabara pia haukuweza kuutambia mwili huo.

Kim Jong-nam anadaiwa kuwa mwanamume aliyefariki wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, baada ya kuonekana kana kwamba alipewa sumu.

Pyongyang imetilia shaka utambulisho wa mwili huo na imeitaka Malaysia kusalimisha mwili huo kwa maafisa wa Korea Kaskazini.

Jumatatu, Malaysia ilimuita nyumbani balozi wake kutoka Korea Kaskazini huku mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ukiendelea kutanda. Kuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasia

Maafisa wa Malaysia wamesema wanahitaji kupata vinasaba kutoka kwa jamaa za Kim Jong-nam ndipo waweze kuutambua mwili huo kikamilifu.

Ulinzi mkali umewekwa katika hospitali ambapo mwili huo unahifadhiwa.

Kuna taarifa kwamba huenda mwanawe Kim Jong-nam, Kim Han-sol, amesafiri Malaysia kuuchukua mwili huo. claim the body.

Jumanne, maafisa wa polisi waliokuwa na silaha kali walifika katika hospitali hiyo ya Kuala Lumpur, na baadaye wakafuatwa na maafisa wa usalama waliokuwa katika magari yasiyokuwa na utambulisho rasmi.

Mwanawe Kim, Kim Han-sol amekuwa akiishi Macau. Mwanamke mmoja alikamatwa kuhusiana na mauaji hayo, na alisema alidhani ulikuwa mchezo wa kuigiza Raia wanne wa Korea Kaskazini wanasakwa na wachunguzi wa jinai kuhusiana na kifo cha Kim
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: