BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANANCHI WAPEWA ELIMU PORI LA AKIBA LA WANYAMAPORI LA RUNGWA

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania-TAWA wakishirikiana na Mradi wa kuhimarisha Mtandao wa Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST) kwa kutumia wataalamu wake inafanya ziara ya kutembelea vijiji vinavyozunguka Pori la Akiba Rungwa Wilaya ya Manyoni.

Ziara hiyo ni kutoa elimu ya wanyamapori kwa njia za mikutano kufuatia maandalizi ya Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo yanategemewa kuadhimishwa jijini Dar es Salaam tarehe 3/3/2017.

Kauili mbiu ya Siku ya Wanyamapori Duniani ni ‘Vijana tushiriki katika Uhifadhi’

Elimu hii katika Wilaya ya Manyoni imeanza rasmi tarehe 18/2/2017 na itachukua muda wa siku kumi na kuhitimishwa tarehe 25/2/2017 inawashirikisha wataalamu wa Maliasili kutoka wilaya ya Manyoni wakiwemo Afisa Misitu na Afisa wanyamapori wa Wilaya ya Manyoni. 


Vijiji vilivyoelimishwa ni kijiji cha Imalampaka, Sasilo na Ipululu. Vijiji vingine ambavyo vimelengwa kuelimishwa ni Simbanguru, Mpapa, Iseke,Nkonko, Damwelu, Doroto na Lulanga.

Msafara huo unaongozwa na Twaha Twaibu ambaye ni Afisa habari na Mahusiano wa TAWA ambaye ameongozana na Herman Nyanda naye kutoka TAWA anayeshughulikia Ushirikishwaji jamii katika uhifadhi, Ramadhani Mdaile kutoka Pori la Akiba Rungwa nayeshughuka na Masuala ya Uenezi, Malima kutoka mradi wa SPANEST na wataalamu wa maliasili kutoka Wilaya ya Manyoni.

Kwenye mikutano hiyo, Twaha aliwaelezea wananchi wa vijiji hivyo faida mbalimbalimbali za wanyamapori, Sheria ya kuhifadhi wanyamapori Na.5 ya Mwaka 2009 inazungumzia vipi suala la wanyamapori wakali na waharibifu, jinsi Serikali inavyowalipa wananchi wake kifuta jasho na machozi baada ya mashamba yao kuharibiwa na wanyamapori na wengine kujeruhiwa au kuuwawa na wanyamapori. 


Na kuwaeleza kuwa Serikali yao kupitia Wizara ya Malaisili na Utalii inawajali sana na kuwaomba wasijihusishe na vitendo vya ujangili wa wanyamapori,

Aidha mtaalam kutoka mradi wa SPANEST Malima Mbijima alieleza kwamba mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiwa na lengo la kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori katika ukanda wa kusini mwa Tanzania unao jumuisha Pori la Akiba la Rungwa.


Pori lingine ni pori la Akiba Mpanga Kipengele, Hifadhi ya Taifa Ruaha na Kitulo, ili wanyamapori hao waweze kuchangia zaidi maendeleo ya jamii katika kizazi cha sasa na vijavyo kupitia utalii na fursa nyingine. Shughuli za Utalii hapa Tanzania zinachangia asilimia 25 ya fedha za Kigeni.

Ramadhani Mdaile akisisitiza suala la kutojihusisha na ujangili wa wanyamapori na ukataji wa mbao katika Pori la Akiba, aliwaeleza kuwa wananchi inabidi waheshimu mipaka ya Hifadhi ya Mapori ya Akiba kwa kuacha mita 500 kutoka hifadhi wanapolima au kufanya shuguli zao.

Mita hizi ziko kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Kuhifadhi wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009.
 

Herman Nyanda kutoka Makao Makuu ya TAWA aliwaelezea wananchi waanzishe maeneo ya hifadhi za wanyamapori (WMAs), na kuwaeleza umuhimu, faida za maeneo hayo kama njia mojawapo ya kunufaika na wanyamapori kwa mfano shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha. 

Maeneo hayo yatatengwa kwenye ardhi ya vijiji vyao kwa kufuata mpango wa matumizi bora ya Ardhi. Maeneo hayo yanawasidia katika ufugaji wa nyuki, kupata kuni, kuhifadhi vyanzo vya maji.

Wataalamu kutoa halmashauri za wilaya ya Manyoni na Itigi walizungumzia ukataji ovyo wa misitu na upasuaji wa mbao ambao haufuati sheria kwamaba unapelekea uharibi wa mazingira katika wilaya yao. 


Na kuwasisitiza kufuata taraibu na sheria za uvunaji wa misitu. Aidha, Afisa wanyamapori wa Wilaya alizungumzia suala ya wanyama wakali na waharibifu wa mazao, pamoja na taratibu za kufuata endapo wanapatwa na matatizo hayo. Alifafanua viwango vya malipo kwa wanachi wanaopatwa na madhara ya wanyamapaori.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: