BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UPINZANI WAPATA PIGO BAADA YA KIONGOZI WAO KUFARIKI DUNIA

Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84.

Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu.

Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake. Tshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRC

Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.

Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: