BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKARDINALI KANISA KATORIKI WAPANGA KUMSHINIKIZA PAPA FRANSIC 16 KUJIUZULU


Papa
Francis wa 16

Jopo la Makardinali waliompa ushirikiano mkubwa Papa Francis wa 16 wakati wa uteuzi wake, wamepanga kumshinikiza ajiuzulu kutokana na ukiukwaji wa maadili ya kanisa.

Gazeti la The Times na Libero la Italia, yameandika kuwa Makardinali hao zaidi ya dazeni, wamepanga kushinikiza Papa Francis ajiuzulu lakini bila kujitenga naye kwa namna yoyote ile. 


Hata hivyo haijafafanuliwa ni maadili gani aliyoyavunja Papa huyo.

Makardinali hao ndiyo waliofanya jitihada kubwa za kuteuliwa kwa Papa Francis katika uteuzi wa nafasi hiyo mwaka 2013. 


Mwandishi Antonio Socci ameandika katika gazeti la Libero na kueleza kuwa kwa sasa Makardinali wanajadili iwapo Papa akijiuzulu nani atashika nafasi yake.CHANZO/MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: