BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA AACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA KUSOKA RUMANDE MIEZI MINNE

Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakishangilia kwa furaha baada ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kuachiwa kwa dhamana mahakama kuu leo jijini Arusha.

Arusha.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, ameachiwa kwa dhama leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Lema ameachiwa kwa dhamana ikiwa ni takribani miezi minne tangu awekwe rumande kwa kesi ya uchochezi.

Polisi wa kutuliza ghasia walijaa mahakamani hapo wakiwafukuza wafuasi wa Lema waliojaa katika viwanja vya mahakama hiyo.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walikuwepo mahakamani hapo leo.Chanzo/Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: