BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIVI NDIVYO ULEVI UNAVYOUA VIPAJI VYA WANAMICHEZO CHIPUKIZI MOROGORO

Baraka Ally (Cha K) akiruka juu na pikipiki aina ya Kawasaki 450 wakati wa michezo ya pikipiki iliyoadhimishwa katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwenye uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Juma Mtanda, Morogoro.
Ulevi umetajwa kuzingua na kudidimiza vipaji vya wanamichezo chipukizi na kupelekea vijana wengi kupoteza mwelekeo na kushindwa kuendeleza vipaji vyao katika michezo ya aina mbalimbali ukiwemo mchezo wa pikikipiki hapa nchini.

Akizungumza na MTANDA BLOG katika mahojiano maalumu mjini hapa , Nahodha wa klabu ya Tanzania Motor Cross Aprobatic ya Dar es Salaam (TMAC), Timtim Rajabu alidokeza kuwa ulevi ndio ukichangia kwa kiasi kikubwa kuporomosha na kupoteza vipaji vingi vya vijana katika kuendeleza michezo.

Timtim ambaye alitua mkoani Morogoro na timu ya waendesha pikipiki za michezo na kutoa burudani katika sikukuu ya Pasaka alisema kwamba ili kijana atimize ndoto yake ya kuendeleza kipaji chake anachotakiwa ni kujiepushe kabisa kujingiza kwenye ulevi wa namna yoyote.

“Mimi nimeishi Morogoro kisha kuhamia jijini Dar es Salaam miaka ya nyuma na sasa ni hahodha wa klabu ya michezo ya pikipiki lakini nimeshangazwa kuona vijana wengi wa Morogoro wamejiingiza kwenye ulevi na kufikia hatua ya kushindwa kumudu kutumia pikipiki za michezo kutokana na kuendekeza ulabu na hii ni noma sana.”alisema Timtim.

Timtim alieleza kwamba wengi wa wachezaji wa mchezo wa pikipiki Morogoro hawawezi kuingia kwenye michezo hiyo pasipo kunywa jambo linalowafanya watu waamini kuwa pombe ndio inayotawala akili na kusipokunywa hawezi kuendesha pikipiki hizo.

Katika michezo hiyo, Ally Ramadhan (Kibogoyo), Francis Francis wa Morogoro walishindwa kumudumu vyema mikimikimi yam bio za Supar Cross wakati wakitumia pikipiki aina ya Honda Beter 250 na KTM 450.

Mchezaji, Masoud Hamis (Chudi 05) aliweza kukonga nyoyo za mashabiki kwa kuongoza mbio za super cross akitumia pikipiki KTM 450 mara mbili akifuatiwa na Clement Clement (Kilikuu) akiwa na Beter 300 wakati Ahmed Yahaya (Kalunde) akitamba na Yamaha 250.

Wachezaji wengine walioshiriki michezo hiyo ni pamoja na Joseph Moshi (Maisha) aliyekuwa akitumia Honda CRF 450, Gabriel Gebo na Honda MD 300 wakati Baraka Ally (Cha K) akitamba na Kawasaki 450.alieleza Timtim.

Timtim alieleza kuwa licha ya mashabiki kuona mbio za supar cross, wachezaji hao walionyesha michezo mingine ya kuruka ubao na kupaa hewani na pikikipi kisha kutua ardhini kwa uhodari mkubwa.

Mashabiki wa mchezo huo muda wote walikuwa wakimsha shangwe kwa mchezaji Chud 05 (Masoud Hamis) namna namna alivyokuwa anamudu vyema mbio za super cross na kuruka ubao na pikipiki aina ya KTM 450 katika michezo iliyofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: