BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KATIBU TAWALA SHINYANGA AWACHIMBIA MKWARA WAUGUZI


KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema watumishi wa afya wenye tabia ya kutoa lugha chafu kwa wagonjwa atawachukuliwa hatua kali za kinidhamu pamoja na kusimamishwa kazi.

Alisema kuwa serikali imechoka kuendelea kusikia kuwapo wahudumu wa afya wenye tabia chafu ya kuwatukana na kutowahudumia ipasavyo wagonjwa, wakati wamepewa mafunzo ya namna ya kutoa hiyo kwa weledi.

Akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa kidini mkoani hapa kuhusu umuhimu wa waumini kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF), Msovela alisema moja ya changamoto inayowakabili sekta ya afya nchini ni baadhi ya watumishi kulalamikiwa kutoa lugha chafu na kutowahudumia ipasavyo wagonjwa.

“Baadhi ya wahudumu wa afya kwenye hospitali zetu hawana uadilifu wa kazi, wamekuwa wakitoa lugha chafu kwa wagonjwa kitendo ambacho tunaonya kwa mara ya mwisho na tutaweka mitego yetu ili atakaye bainika kuendeleza tabia hiyo atupishe na hakutakuwa na huruma,” alisema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: