BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA WILAYA ATOKA SALAMA MIKONONI MWA HAKIMU MAHAKAMA YA BUNDA

Simoni Odunga  

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara imemwachia huru Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Simoni Odunga aliyekuwa anashitakiwa kwa tuhuma za wizi wa kuaminiwa pamoja na kutoa lugha ya matusi kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi.

Odunga alikuwa anashitakiwa na mwanamke mmoja Veroline Odhiambo, aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa kijiji cha Bukore wilayani Bunda, ambapo kesi hiyo namba 65 ya mwaka 2016, ilianza kusikilizwa mahakamani hapo mwaka jana.

Alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ambayo ni pamoja na wizi wa kuaminiwa wa Euro 2,758 (Sh milioni 5.8), pamoja na kosa la lugha ya matusi kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, chini ya kifungu Namba 20 kidogo cha kwanza A na cha pili cha sheria ya makosa ya mtandao.

Mahakama hiyo imemwachia huru mkuu huyo wa wilaya baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani, katika makosa yote mawili.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda, Jacqueline Rugemalila alisema katika kesi hiyo, upande wa mashitaka umeshindwa kuleta ushahidi unaojitosheleza kwa ajili ya kumtia hatiani mshitakiwa huyo.

Alisema kila upande ulileta mashahidi wanne, na baada ya kusikiliza kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mahakamani hapo mwaka jana na kisha kupitia ushahidi wa pande zote mbili, amebaini kuwa mshitakiwa huyo hakutenda makosa hayo na hivyo mahakama hiyo inamwachia huru.

Hakimu Rugemalila alisema kuwa hati ya mashitaka ilionesha alipewa kiasi kingine cha Euro, huku ushahidi ukionesha alipewa kiasi kingine, huku pia ukiwa hauoneshi alipewa kwa matumizi gani na kwamba pia hakuna ushahidi unaoonesha mshitakiwa alikuwa ni wakala wa mlalamikaji kama ilivyodaiwa na upande wa mashitaka.

Alisema pia upande wa mashitaka ulishindwa kuithibitishia mahakama hiyo mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa simu, kwani namba ya simu inaonekana kwa aliyeutuma ujumbe huo, lakini aliyetumiwa namba hiyo haionekani. 


Hakimu Rugemalila alisema kuwa kwa msingi huo ushahidi haujitoshelezi na hauwezi kumtia hatiani mshitakiwa huyo anayedaiwa kufanya makosa kati ya Desemba mwaka 2014 na Novemba mwaka 2015
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: