BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOMBORA LA KOREA KASKAZINI LASHINDWA KUFYATUKA NA KUPAA ANGANI


Korea Kaskazini imejaribu kufyatua kombora moja lakini likakosa kupaa angani, siku moja tu baada ya kuonya Marekani kuwa haiogopi vitisho vyake vya kivita.

Jeshi la Marekani lilisema kuwa kombora hilo lililipuka sekunde chache baada ya kufyatuliwa katika ufuo wa Mashariki wa Korea Kaskazini.

Afisa mmoja wa Marekani alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora hilo halikuwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine.

Rais Trump alifahamishwa juu ya jaribio hilo lililofanywa masaa machache kabla ya Makamu wa Rais Mike Pence kuwasili Korea Kusini, kwa mashauri kuhusiana na Pyongyang na mipango yake ya makombora ya kinyukilia.

Hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani imekuwa ikipanda, huku kila upande ukijigamba jinsi utakavyoweza kuchafua upande mwingine.

Mnamo Ijumaa Uchina iliitisha mkutano unaonuia kutuliza uhasama huo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: