BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SALMA KIKWETE AAPISHWA RASMI NA SPIKA WA BUNGE KUWA MBUNGE KATIKA BUNGE LA TANZANIA

Salma Kikwete mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai leo amemuapisha mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Rashid Kikwete kuwa mbunge wa Bunge wa kuteuliwa.

Mh.Salma aliandamana na mumewe rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye uwepo wake ulisababisha kelele za shamra shamra kutoka kwa wabunge wakisema kwa sauti 'tumekumiss tumekumiss'.

Mkutano wa saba wa bunge la Tanzania umeanza kikao chake cha kwanza cha mkutano wa bajeti hii leo.

Mama Salma kama anavyotambulika na wengi nchini ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: