BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BODI YA USAJILI YA MAKANDARASI (CRB) YAWATUMBUA MAKANDASI 4,500 TANZANIA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani kushoto.

MAKANDARASI 4,578 wamefutiwa usajili katika Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kukiuka taratibu nyingine zinazoongoza shughuli za ukandarasi.

Hayo yalibainishwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkenge (CCM), Dk. Diodorus Kamala.

Katika swali lake, Kamala alitaka kujua tangu kuanzishwa kwa CRB ni makandarasi wangapi Watanzania wamesajiliwa na taasisi hiyo na serikali na halmashauri za wilaya zinatumia vigezo gani kutoa kazi kwa makandarasi.

Akijibu swali hilo, Ngonyani alisema tangu ilipoanzishwa mwaka 1997 imesajili jumla ya makandarasi wa Kitanzania 13,513 ambapo kati yao 8,935 usajili wao uko hai na 4,578 wamefutiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kukiuka taratibu na kushindwa kulipa ada.

Alisema vigezo vinavyotumiwa na serikali katika utoaji wa zabuni kwa makandarasi vinazingatia matakwa ya sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011.

Aidha katika swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Cecilia Pareso, alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwalipa makandarasi fedha wanazoidai kwa kuwa wanadai fedha nyingi na kuwafanya washindwe kutekeleza majukumu yao.


Akijibu swali hilo, Ngonyani alisema hadi sasa zaidi ya Sh.Bilioni 700 zimelipwa kwa makandarasi na wanaendelea kukamilisha kulipa kiasi kilichobaki/Nipashe.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: