BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHELSEA NA HESABU ZA NGUVU KUMSAJILI MSHAMBULIAJI WA BAYERN MUNICH, ROBERT LEWANSOWSKI

Mabingwa wa England Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Poland na Bayern Munich Robert Lewandowski, 28 (Daily Mirror).

Tottenham wanataka pauni milioni 45 kumuuza beki Kyle Walker, 27, ambaye anasakwa na Manchester City (Daily Star).

Arsenal wamewaambia Barcelona kuwa beki wake Hector Bellerin, 22, hauzwi na wana uhakika mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain atabakia Emirates (Independent).

Arsenal wanajiandaa kutoa euro milioni 30 kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan (Marca).Arsenal lazima wasubiri mpaka michuano ya Kombe la Shirikisho la Mabara la Fifa imalizike ili kufahamu msimamo wa Alexis Sanchez kuhusu mustakbali wake Emirates (Evening Standard).

Arsenal pia wameanza mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo Aaron Ramsey, 26, ili kuondoa utata wowote kuhusu mustakbali wake (Daily Telegraph).

Real Madrid wanafikiria kumsajili Alexis Sanchez, ili kuziba nafasi ya Cristiano Ronaldo (Don Balon). Alexis Sanchez

Juventus nao wanamtazama beki wa Arsenal Hector Bellerin (Tuttosport).

Juventus pia wanamtaka beki wa Manchester United Matteo Darmian, 27, kuziba nafasi ya Dani Alves, ambaye anatazamiwa kuondoka Italy (Goal.com).

Dani Alves, 34, yuko tayari kusaini mkataba wa miaka miwili na Manchester City, mara atakapokamilisha mazungumzo yake na Juventus (Daily Mail).

Manchester United itakuwa kimbilio pekee kwa Cristiano Ronaldo iwapo ataondoka Real Madrid, kwa mujibu wa washauri wake (Daily Record).

Lakini rais wa Real Madrid Florentino Perez ameelezea sakata la mustakbali wa Ronaldo kama "la kushangaza" na kusema hakuna mipango ya kumuuza mchezaji huyo (TalkSport).
Real Madrid wanafikiria kumchukua N'Golo Kante (kushoto) kutoka Chelsea (Don Balon).

Manchester United hawajakata tamaa ya kumfuatilia mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, lakini watalazimika kulipa hadi pauni milioni 90 (Mirror).

Manchester United hawatoongeza dau lao la pauni milioni 26.4 ili kumsajili kiungo Ivan Perisic wa Inter Milan, na wana uhakika wa kukamilisha mkataba huo (Calciomercato.com).

Liverpool huenda wakakamilisha usajili wa Mohamed Salah siku ya Jumatano - leo- (Sky Sports).

Usajili mpya wa Liverpool Mohamed Salah anataka kuvaa jezi namba tisa (Liverpool Echo).

Swansea watamsajili mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 19, kwa mkopo wa mwaka mmoja (Daily Mirror).

Swansea pia wamemuulizia beki wa zamani wa Liverpool Martin Skirtel, 32, anayechezea Fernabahce (Daily Mail).

Wakala wa Zlatan Ibrahimovic Mino Raiola amesema mchezaji huyo ameitwa na timu nyingi kutoka Marekani na kwingineko (Gazzetta dello Sport).

West Ham wameanza mazungumzo ya mkataba mpya wa kiungo wao Pedro Obiang, 25, ili kuzuia Everton, Sevilla na AC Milan zinazomfuatilia (Daily Mirror).

Chelsea na Atletico Madrid wameanza mazungumzo kuhusu mkataba wa pauni milioni 50 wa usajili wa Diego Costa. Ingawa Atletico wamefungiwa, watamrejesha Costa kwa mkopo hadi Januari adhabu yao itakapomalizika (Mirror).

Chelsea wanamfuatilia winga wa Leicester City Riyad Mahrez, wakati Conte akitaka kuimarisha safu ya ushambuliaji (Evening Standard).

Chelsea wanapanga kumtoa kwa mkopo Kurt Zouma msimu unaokuja, wakati wakijiandaa kumsajili Leonardo Bonucci, 30 kutoka Juventus na Virgil van Dijk, 25, kutoka Southampton (Evening Standard).

Chelsea wamekubaliana mkataba wa mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki kumrejesha Romelu Lukaku Darajani kutoka Everton (Daily Star). Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku

Chelsea wanakaribia kumsajili winga wa Middlesbrough Adama Traore, 21 (Daily Star).

West Brom wanajiandaa kumpa mshahara wa pauni 100,000 beki wao Jonny Evans, 29, na kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo (Sun).

West Brom wametoa dau la pauni milioni 12 kumtaka mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez, 27, ingawa Burnley na Newcastle pia zinamtaka (Daily Mail).

Beki wa Real Madrid, Pepe, 34, anasema hajaamua kuhusu mustakbali wake, licha ya kuhusishwa na kuhamia PSG (ESPN FC).

Inter Milan wamemuulizia kiungo wa Barcelona Andres Iniesta ambaye mkataba wake unamalizika mwakani (Gazzetta).

Beki wa Manchester City, Eliaquim Mangala, 26, yupo kwenye mazungumzo ya kuhamia Lyon (Daily Mail).

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema mshambuliaji Olivier Giroud, 30, bado ni mchezaji muhimu katika kikosi chake (Evening Standard).

Winga wa Watford Nordin Amrabat, 30, amehusishwa na kuhamia Deportivio la Coruna (Watford Observer).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Tetesi za soka barani Ulaya na Salim Kikeke

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: