BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DONALD TRUMP APATA PIGO LINGINE MAREKANI


Mahakama ya rufaa nchini Marekani imemua kuwa uamuzi wa kuzuia mpango uliofanyiwa marekebisho wa marufuku ya Rais Donald Trump kuzuia watu kutoka nchi sita za kiislamu utasabaki kuwepo

Wakitoa hukumu kufuatia kesi iliyowasilishwa na hjimbo la Hawaii, majaji walipata kuwa amri hiyo kuiu inakiuka sheria zilizopo za uhamiaji.

Rufaa hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Fransisco, ni kufuatia umamuzi uliotolewa kupinga raia wengi wao wakiwa kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani.

Hata hivyo mahakama haikusema kuwa serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi kwa watu wanaoingia nchini humo.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa rais Trump,akisistiza kuwa kila lilalowezekana linatakiwa kufanywa kwaajili ya ulinzi wa Marekani

"Nadhan wote tunafahamu kuwa hizi ni nyakati za hatari dhidi ya tishio la ugaidi,tunapaswa kuwa kulinda kuingia kwa watu wanaoweza kufanya vitendo vya ugaidi na uwagaji wa damu.Tunaendelea kuwa na Imani kwamba amri za rais wetu ni kwa mjibu sheria na kwamba tunaamini mahakama ya juu itazipitisha"

Hata hivyo mwanasheria mkuu wa jimbo la Maryland na Columbia Brian Frosh amefungua mashitaka dhidi ya rais Trump kwa madai ya kupokea malipo ya nje kupitia makampuni yake.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, Frosh Mwana Maryland's Attorney Generel, Brian Frosh, ameseama Trump kujihusisha biashara akiwa madarakani ni kuvunja katiba

"Aliiteuwa Hoteli yake ya kimataifa ya Trump kwaajili ya wanadiplomasia na maofisa wa serikali. Amekuwa akionekana kwenye sehemu nyingi za biashara zake na imekuwa kama sehemu ya kutangaza biashara hizo.


Analipwa na makampuni yanayo milikiwa na nchi za nje kama vile China ambao pia ni wapangaji katika majengo yake.Na amekuwa akiendelea kuchukua malipo kutoka nchi za Saudi Arabia, India, Afghanistan na Qatar nchi ambazo zina hisa majengo yake ya kibiashara yajulikanayo kama Trump World Tower.

Rais Trump amekuwa akikabiliwa na upinzani mkali kufuatia baadhi ya maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya tangu kuingia madarakani,ikiwemo hatua hii aliyoichukua kupiga marufuku raia kutoka baadhi ya nchi za Kiislam kuingia Marekani
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: