BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHAKAMA KUU YARUHUSU KURA YA SIRI YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS

Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imeamuru kuwa kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma inaweza kufanywa kwa siri.

Mahakama ya katiba ilisema kuwa spika wa bunge na haki ya kuamuru hatua kama hiyo. Awali alisema kuwa hakuwa na mamlaka kama hiyo.

Vyama vya upanzani vinaamini kuwa chini ya kura ya siri, wabunge kutokaa chama cha Zuma cha ANC wanaweza kupiga kura ya kumpinga.

Zuma aliponea kura za awali ya kutokuwa na imni naye, rais Zuma amekuwa chini ya shinikizo kufuatia shutuma nyingi ikiwemo madai ya ufisadi na mabadiliko kwa baraza la mawaziri yaliyokumbwa na utata.

Akitoa uamuzi huo Jaji mkuu Mgoeng Mgoeng, alisema kuwa spika wa bunge ana mamlaka ya kuamua ni njia gani kura hiyo itafanyika.

Spika wa bunge Baleka Mbete ni afisa wa cheo cha katika chama cha ANC na alikuwa amedai kuwa sheria za bunge haziruhusu kufanyika kura ya siri, lakini sasa tarehe mpya ya kura hiyo ya kutokuwa na imani itatangazwa.BBC
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment