BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA MWINTANGA CUP 2017 YAFIKIA HATUA YA PILI MOROGORO


Juma Mtanda, Morogoro.
Mashindano ya soka ya Mwintanga Cup 2017 ya kuwakumbuka na kuwarehemu wanamichezo waliofariki dunia, yamefikia hatua ya pili baada ya kumalizika kwa michezo ya awali yaliyoanza kutimua vumbi Mei 5 mwaka huu ikishirikisha timu 58 kwenye uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Baadhi ya wanamichezo hao ni, Salum Mwintanga aliyekuwa Katibu mkuu chama cha soka Morogoro huku Mohamed Msomali, Hamis Mwinchumu, Hashim Mkingie wakiwa katika nafasi ya ukocha, Mohamed Bakari (Mzee wa Kubalansi) Mwamuzi, wakati Idrisa Ngulungu na Boniface Njohole wakiwa wachezaji.

Wachezaji hao na wengine walikuwa hazina kubwa kwa taifa huku wakiacha historia mbalimbali katika soka.


Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Katibu Mtendaji wa chama cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande (Pichani) alisema kuwa michezo hiyo ilianza kwa mchezo kati ya Mwere Kids dhidi ya Home Boys ikichezwa kwa mtindo wa mtoano.

Maharagande alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michezo ya awali, timu 30 zimetinga hatua ya pili ya mashindano hayo huku Stend Hiace FC ikijitupa uwanjani kufungua pazia na Karume Rangers kwa mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ya pili.

Alitaja timu zilizofuzu hatua hiyo kuwa ni Young Stars FC, Home Boys FC, Stend Hiache FC, Karume Rangers FC, Masubo United, Jamaica FC, Miembe Mitatu FC, Kihonda Magholofani FC, Talent United, JL Team FC, G.Seven FC, Moro Kids SC, Kivuma United.

Nyingine ni Even, Jordan University FC, Don Bosco FC, Chicago FC, Barcelona FC, Chamwino Youth SC, Chipolopolo FC, Mandale United, Kasanga United, Umoja wa vijana ccm FC, Magadu, Black Fighater, Msamvu City FC, Chicago ya Wagogo FC, Chamwino Market FC, Chamwino Rangers FC, Dawa Yao SC na Moro City FC.

Maharagande alisema kuwa pazia la mzunguruko wa lilifungwa Juni 11 kwa mchezo kati ya Chicago FC dhidi ya ST.Patrick ambapo Chicagi iliwalaza wapinzani wao kwa bao 1-0 lililofungwa na Hassan Ally katika dakika 66.

Maharagande alisema kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atazawadiwa seti mbili za jezi huku mshindi wa pili seti moja ya jezi na mshindi wa tatu akiambulia mipira mitano.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: