BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHANGA WA MADINI, CCM YARUSHA DONGO ZITO KWA UPINZANI NA KUWATAKA KUDANDIA TRENI KWA MBELE


Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula

Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula amesema kitendo alichokifanya Rais John Magufuli cha kuwafichua wanaotorosha mchanga wa madini kipo kwenye ilani ya chama hicho hivyo wapinzani waache kudandia treni kwa mbele.

Mangula amesema hayo leo (Jumamosi) wakati akizungumza na wanachama wa CCM kwenye kongamano la kuunga mkono juhudi za Rais na kumpongeza kwa kuwafichua mafisadi lililoandaliwa na wanachama hao.

"Alichokifanya Rais kipo ndani ya ilani ya chama, wapo wanaotaka kudandia treni kwa mbele wakidai wao ndiyo walikuwa na mawazo hayo, nataka niwaambie Rais anatekeleza ilani hiyo ni mipanngo ya CCM, "amesema.

Pia, Mangula amewaonya watu wanaoibuka na kutaka kukwamisha kazi anayofanya Magufuli kuwa hawataweza na nchi haitashtakiwa kama wanavyodai. 


“Niwatoe hofu wananchi na wanachama wote kuwa nchi iko salama zaidi tumuunge mkono Rais wetu kuwafichua wezi wa mali za nchi, "amesema/Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment