BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKE WA WAZIRI MKUU APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA


Mke wa waziri mkuu aliyechaguliwa nchini Lesotho ameuwawa siku mbili kabla ya kuapishwa kwake.

Polisi wanasema mke wa Thomas Thabane, Lipolelo, ambaye walikuwa wametengana aliuwawa hapo jana Jumatano wakati akiendesha gari karibu na nyumbani kwake, katika mji mkuu wa Maseru.

Hawajakuwa wakiishi pamoja tangu mwaka 2012, baada ya Bwana Thabane kuwasilisha kesi ya talaka mahakamani.

Lesotho imekuwa na historia ya migogoro ya kisiasa, mnamo mwaka mwaka 2014 wanajeshi walijaribu kumpindua Bwana Thabane, pale alipokuwa waziri mkuu.

Lipolelo alishinda kesi dhidi ya mumewe wakati akiwa waziri mkuu, akitaka awe na cheo cha mama wa taifa, baadala ya mke wake mdogo Liabiloe Thabane.

Uchaguzi ulifanyika nchini Lesotho mapema mwezi huu na ndio wa tatu katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na mgogoi mbaya wa kisiasa.

Bwana Thabane ataapishwa siku ya Ijumaa.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment