BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMFALME APOKONYWA TAJI NA KUFUTWA KAZI UWAZIRI WA MASWALA YA NDANI

 

 

KUTOKA MASHARIKI YA KATI, HAMKANI SI SHWARI TENA. 

Na Geofrey Chambua.
Mfalme Salman wa Saudia amebadilisha mkondo wa urithi na kumfanya mwanawe wa kiume Mohammed bin Salman kuwa mwanamfalme na kuwa wa kwanza kumrithi.

Aliyekuwa mwanamfalme, Mohammed bin Nayef amepokonywa taji lake na kufutwa kazi kama waziri wa maswala ya ndani.

Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 ataendelea kuwa waziri wa ulinzi mbali na kuwa naibu waziri mkuu.

Mfalme wa sasa Salman bin Abdulaziz ndio mtawala wa mwisho kutoka watoto wa mwaasisi wa ufalme huo Abdualiziz bin Saud. Kuteuliwa kwa mwana mfalme huyo kuwa mrithi wa kiti cha ufalme imeonekana kama Mapinduzi dhidi ya kurithi ufalme huo kwani wakati Mfalme Salman alipochukua Kiti hicho mwaka 2015 alimteua Prince Mohamed Bin Nayef kuwa mrithi wake.

Mohamed bin Salman ni mtu ambaye ameleta utata mkubwa kwenye sera za nje za nchi hiyo kwani mpaka sasa anaendesha vita dhidi ya Yemen na ametishia kuanzisha vita na Iran. Pia anadaiwa ndio muhusika mkuu kwenye mgogoro wa Qatar na Saud Arabia.

Uko wa kifalme wa Saud Arabia unakisiwa kuwa idadi ya watu 15000 lakini wenye utajiri mkubwa kwenye familia hiyo inakisiwa ni watu 2000.

Somehow, japo ufalme umerudi kwa mlango wa dini. Mwenye Iran ni Ayatollah Khomein (kiongozi mkuu wa dini); huyo rais anayechaguliwa "kidemokrasia" ni maigizo tu; huwekwa pale na Ayatollah na hana say yoyote zaidi kuwa mtii kwa Ayatollah na kuzingatia maagizo yake.

NITARUDI KUWALETEA UNDANI WA SAKATA LENYEWE ILA PICHA IKUPE TAFAKURI YA KINACHOENDELEA HUKO MASHARIKI YA KATI
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment