BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AWACHARUKIA WANAOUNGA USHOGA, HAKUNA KUSOMA MWANAFUNZI ALIYEBEBA UJAUZITO

Rais Dk John Magufuli ameeleza kuwa katika utawala wake hakuna mwanafunzi aliyebeba ujauzito atarudi shuleni na kuendelea na masomo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo Mkoani Pwani, Dk Magufuli alisema kuwa kitendo cha kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kisha kurejea darasani kuendelea na masomo inaweza ikafikia kipindi darasa zima lina watoto na mwalimu kujikuta akifundisha na wao kutoka nje kwa ajili ya kwenda kunyonyesha.

Rais Magufuli alisema kuwa hata kama ni watoto wangu, yaani ampeleke shule alafu apate mimba kisha nimrudishe shuleni ? alihoji na kutoa tahadhari mwanae aende akapate mimba kisha aone kama ataweza kumrudisha shule !.

"Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea."alisema Rais Magufuli.

Rais Magufulia alisema kuwa wakati mwingine ukizikiliza NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya na ndani ya utawala wake haitotokea jambo hilo.

"Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi lakini serikali haiwezi kuwasomesha katika mfumo huo"alisema Rais Magufuli.

Alisema Rais Magufuli kuwa hao wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu, Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Katika hatua nyingine rais Magufuli amechukiwa na mapenzi ya jinsi moja na kuwataka watanzania kutoiga mambo yasiyo na manufaa.


"Huku kuigaiga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai, tunaweza kujiuliza wamekuwa wakija na misaada ambayo ni mali zetu ambazo wametuibia."alisema Rais Magufuli.

Kuna mambo ya kujiuliza...Nyie wafugaji mmefuga mifugo wa kila aina lakini je mmejawahi kuona hata mbuzi au ng'ombe amekosea siku mmoja kumwingilie jike kinyume na maumbile ?....lakini wao wanataka Watanzania wakosee katika hilo.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment