BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI KUOMBEWA DUA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

Rais Dk John Magufuli.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
Viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya siasa na serikali wanatarajia kukusanyika kwenye ibada maalumu ya kumuombea dua njema, Rais Dk John Magufuli kutokana na hatua anazochukua dhidi ya wabadhirifu wa rasilimali za nchi inayofanyika leo saa 4 asubuhi uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

Akizungumza na MTANDA BLOG ofisini kwake, Kamanda wa jeshi la polisi Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa jeshi hilo limepokea ombi la mkusanyiko wa viongozi hao pamoja na waumini wao kwa lengo la kumuombea dua njema rais Dk Magufuli.

Matei alisema kuwa tayari jeshi hilo limejipanga ili kuhakikisha linatoa ulinzi na usalama katika mkusanyiko huo wa maombizi hayo.

“Jeshi la polisi limejiandaa kutoa ulinzi na usalama kwa viongozi na waumini katika ibada maalumu ya kumuombea dua njema amir jeshi mkuu rais Dk John Magufuli kama maombi ya mkusanyiko huo tulivyopokea.”alisema Kamanda Matei.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris alisema kuwa CCM imeandaa mkusanyiko huo kwa lengo la kukusanya dua za pamoja ili kumuombea jemedari mkuu rais Magufuli afya njema ili aongezewe ujasiri, afya njema na mwenyezi mungu.

Kalogeris alisema kuwa Dk Magufuli amekuwa akifanya kazi ngumu za kupambana na kurejesha uchumi wa taifa na hilo limeonyesha njia nzuri na amethubutu kikamilifu katika kuirejesha nchi katika heshima yake dhidi ya wabadhirifu wa mali za umma.

“Tumeona kama chama tawala CCM kumuombea dua njema kwa mwenyezi mungu ili amuepushe na shari ya kila namna na kumpa afya njema ili alitumikie taifa na sisi kama viongozi kwa nafasi zetu tutahakikisha tunamuunga mkono kwa njia moja ama nyingine.”alisema Kalogeris.

Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge alisema kuwa ibada itaanza saa 4 asubuhi na itaongozwa na viongozi wa dini zote.

Milonge alisema kuwa tayari wamealika viongozi wa siasa, dini, wazee wa mila na serikali ili kwa pamoja waongooze dua kwa rais Dk John Pombe Magufuli katika uwanja wa jamhuri Morogoro.

“Dua itaanza saa 4 asubuhi na itaongozwa viongozi wa dini wakishirikiana na wazee wa mila lakini tumealika viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Morogoro, wenzetu wa Cahdema na wananchi wa kawaida kuhudhuria dua hii.”alisema Milonge.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: