BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SABABU ZA DIEGO COSTA KUACHWA KWA NJIA YA MESEJI NA KOCHA WA CHELSEA

 

Na Geofrey Chambua 
1. Tofauti na wachezaji wengi ambao hupitia academy za soka, Diego alijifunzia soka mtaani kwa kucheza chandimu. Baada ya kuiva kisoka alichukuliwa na timu ya Barcelona Esportiva Capela, ambayo ilikua inahamasisha vijana wa mitaani kucheza soka badala ya kutumia madawa ya kulevya..hapo alianza na posho ya $100 kwa mwezi

2. Diego Costa alianza utukutu tangu akiwa na umri mdogo tu, alifungiwa kucheza soka kwa miezi minne baada ya kumchapa kbao mchezji wa timu pinzani tena mbele ya mwamuzi, wakati huo akichezea Barcelona Esportiva Capela


3. Kwa nyakati fulani, Diego alipelekwa kwa mkopo timu ya Albacete ambayo ni ya daraja la chini huko Uspain, hapo akagoma kufanya mazoezi baada ya kugundua kwamba wafanyakazi walikua hawalipwi ..hapo pia anahusishwa kutaka kumteka daktari wa timu kwa kutumia mto wa hotelini hapo.

4. Diego anajulikana sana kwa utundu wake uwanjani na takwimu zinaonesha kwamba ameshalamba njano 58 na Nyekundu 7 hadi sasa. Mwaka 2015, Gazei moja la Spain lilimitaja kama mchezaji anayechukiwa kuliko wote uwanjani kwa utukutu wake na wachezji wengi wamekiri kumkwepa sana wawapo uwanjani kwa tabia zake za kuwagonga vichwa refa awapo mbali.

5. Licha ya upinzani mkali wa kisoka na licha ya kwamba Baba yake ni mzaliwa wa Brazil, yeye mwenyewe aliamua kumpa Jina la Diego kuakisi mchezaji wa Argentina Diego Maradona .....zaidi sana baada ya kuichezea Atletico Madrid kwa miaka 5 mfululizo, Diego alistahili hati ya Spain na hapo ndipo alipoamua muichezea Spain badala ya Brazili ya kwao. Hata hivyo amechezea timu ya Brazil MECHI MBILI TU

6. Japo aliwaniwa pia na Arsena, ilikua rahisi sana kwa Jose kumchukua Chelsea sababu ni moja tu kwamba Jose na Diego wakala wao ni mmoja akiitwa Jorge Mendes.

7. MWAKA 2014, Diego da Silva Costa alijiunga na Chelsea akitokea Atletico Madrid ya Hispania. Sasa ni misimu mitatu na tayari amebeba makombe matatu akiwa na klabu hiyo ya London, England. Katika mechi 87 akiwa na Chelsea, amefunga mabao 52, Kati ya hayo, Magoli 5 amefunga kwa kichwa, 34 kwa mguu wa kulia, 13 kwa guu la kushoto na moja kwa tuta. Amepiga pasi 2,566 na majalo 45.

LICHA YA YOTE HAYO; Hivi karibuni, Costa ametoa siri hadharani kwamba huu ni msimu wake wa mwisho na Chelsea kwa kuwa tayari ametumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kocha wake, Antonio Conte ukimueleza kwamba hamhitaji tena.

Sababu za wazi zinazotajwa kuachwa kwa Costa ni pamoja na Ubabe uliopitiliza, Ubishi, kuenda sana ngada na chabo, uvivu wa mazoezi na kubwa kabisa kuwa chakari muda mwingi na mbaya zaidi kukutwa na pombe kwenye chumba cha maadalizi ya mechi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment