BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA HISPANIA YAMKASIRISHA CRISTIANO RONALDO, KUIHAMA KLABU YA REAL MADRID


Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekereka sana baada ya tuhumiwa kwamba alifanya ulaghai wakati wa ulipaji ushuru na anataka kuihama klabu hiyo, duru zimeiambia BBC.

Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanamtuhumu Ronaldo, 32, kwa kutumia ulaghari kutolipa mamilioni ya ushuru.

Amekanusha tuhuma hizo.

"Anahisi kwamba amekuwa mkweli, ana sifa nzuri na alifanya kila kitu ipasavyo," ameongeza mdokezi.

Mkataba wa Ronaldo katika klabu hiyo ya Madrid una kifungu cha euro bilioni moja (£874.88m), ambacho kinafaa kufikishwa ndipo afunguliwe kutoka kwa mkataba wake.

Mdokezi aliongeza: "Amehuzunika sana na ameudhika kwa kweli."

kumfungua kutoka kwa mkataba huo wake.

"Hataki kukaa tena Uhispania. Kwa sasa, anataka kuondoka."

Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa £80m, alitia saini mkataba wa miaka mitano katika klabu hiyo Novemba mwaka 2016.

Mreno huyo anaweza kwenda China, lakini washauri wake wangependa aendelee kucheza soka Ulaya, pengine ahamie Paris St-Germain ya Ufaransa au arejee Ligi ya Premia.

Ronaldo, aliyewasaidia Real kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhumiwa kulaghai maafisa wa serikali ushuru wa takriban euro 14.7m (£13m; $16m) kati ya 2011 na 2014.

Real Madrid wametoa taarifa wakisema wana imani kamili na mchezaji wao huyo, na kwamba wana uhakika atathibitisha kwamba hana makosa.

Msimu wa 2016-17, Ronaldo alisaidia Real kushinda taji la ligi Uhispania wka mara ya kwanza tangu 2012, na pia kutetea taji lao la Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

Ronaldo, aliyeshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya pia akiwa na Manchester United mwaka 2008, amefunga mabao 105 katika michuano hiyo, 11 zaidi ya mpinzani wake wa Barcelona Lionel Messi.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment