BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAEKWONDO YATUMIKA KUVUTA WANAFUNZI KATIKA MAFUNZO YA KUSOMA VITABU MAKTABA MORO

Mwalimu wa mchezo wa taekwondo, Min Ju Kim akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi baada ya kumalizika kwa mafunzo ya matumizi ya maktaba kwa wanafunzi ya kutumia vitabu na mchezo wa taekwondo yaliyofanyika maktaba ya mkoa huo/Juma Mtanda.


Juma Mtanda, Morogoro.
Shirika la kimataifa la Korea International Cooperation Agency limendesha mafunzo ya kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi kutambua matumizi ya maktaba na kupenda kusoma vitabu huku mchezo wa Taekwondo ukitumika kama sehemu ya kivutio cha kuwashawishi katika mahudhuria Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Mwendeshaji mkuu wa mafunzo hayo, Ja Young Lee alisema kuwa wametumia mbinu ya mchezo wa Taekwondo kuwavuta wanafunzi kuhudhuria kwa uwingi mafunzo haya ya kupenda kusoma vitabu katika maktaba na matumizi yake.

Ja Young alisema kuwa licha ya kutumia Taekwondo kama njia ya kuwavuta wanafunzi kuingia katika mafunzo hayo pia wametafsiri vitabu 50 yenye masomo mbalimbali pamoja na hadithi kutoka lugha ya Kingereza kwenda Kiswahili.

“Tupo katika program ya “Tanzania ya Kesho” lenye lengo la kuwajengea wanafunzi kupenda kujua historia mbalimbali lakini hawawezi kujua hilo bila kupenda kusoma vitabu katika maktaba kuu za mikoa na mafunzo hayo yamefanyika Dodoma na tunaendelea hapa Morogoro.”alisema Ja Young.
Mwalimu wa mchezo wa taekwondo kutoka chuo cha polisi academy Dar es Salaam, Andrew George akitoa mafunzo ya kupiga ngumi kwa wanafunzi baada ya kumalizika kwa mafunzo ya matumizi ya maktaba kwa wanafunzi ya kutumia vitabu na mchezo wa taekwondo yaliyofanyika maktaba ya mkoa huo.

Ja Young alisema kuwa mpaka sasa tayari wakutubi 18 wamepata mafunzo ya kuwahudumia wanafunzi kutumia maktaba na kujisomea vitabu ambapo wakutumia 11 wakitoka Dodoma na saba Morogoro.

Ja Young alifichua siri kuwa, kuna tatizo kwa wanafunzi wengi kushindwa kuingia maktaba na kusoma kwa sababu vitabu vingi vya watoto vimeandikwa katika lugha ya kiiengereza, hivyo hawawezikusoma vizuri lakini baada ya utafiti vimeanza kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili fasaha.

Kwa upande wa, mwalimu Min Ju Kim na Andrew George walisema kuwa mchezo wa taekwondo ni mchezo mzuri unaofundisha nidhamu na kujihami na adui pindi mtu anapokushambulia.

Kim alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kuwahamasisha wanafunzi wa kitanzania kupenda kusoma vitaba katika maktaba ili kujua historia mbalimbali lakini watoto wameonyesha kushika mafunzo yote.

“Mchezo wa Taekwondo ni miongoni mwa utamaduni wa watu wa Korea tumekuwa tukijifunza tangu utoto wetu kama sehemu ya kutujenga kinidhamu, kulinda pele adui anapotushambulia lakini kutujenga kiafya, kiakili na kujenga mwili wenye ukakamavu.”alisema Kim.

Mafunzo hayo ya wiki tatu kupitia programu ya Tanzania ya Kesho yalifanyika katika maktaba ya mkoa wa Morogoro na Dodoma yakiendeshwa na wawezeshaji, Ha Yong Lee na Ja Young Lee kutoka maktaba za mikoa hiyo.


Mkutubi Mkuu wa Maktaba ya Mkoa wa Morogoro, Edward Fungo alisema kuwa mafunzo hayo kama uongozi wa maktaba, tayari wameunga mkono kwa kutoa fursa kwa wanafunzi wa shule za msingi kusoma bure kwa siku za jumamosi kuingia maktaba na kusoma vitabu.

Fungo alisema kuwa walipoanza mafunzo hayo wanafunzi walihudhuria wachache lakini baada ya kuwepo kwa mchezo wa Taekwondo wanafunzi wengi wamekuwa wakijitokeza na kufikia 40.

“Kitendo cha vitabu vya kingereza kutafsiliwa kwa lugha ya kiswahili fasaha itatusaidia sana sisi wanafunzi kusoma vitabu vingi kutoka maktaba yetu ya mkoa wa Morogoro tofauti na hapo awali lugha ya kingereza imekuwa kikwazo.”alisema Ally Hassan wanafunzi wa darasa la nne shule ya Msingi Mwere A.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment