BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TANZANIA YAPOTEZA SH 188 TRILIONI KIPINDI CHA MIAKA 19 KATIKA MADINI YA DHAHABU NA SHABA

Tanzania imepoteza takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola milioni 84 za Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba.

Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi March mwaka huu na Rais John Magufuli.

Ripoti hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya kwanza iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa mchanga wenye madini.

Kamati hii ya sasa iliundwa na wataalam wa masuala ya uchumi na wanasheria ambao walikuwa na jukumu la kutazama mikataba ya madini na athari za kiuchumi kwa Tanzania.

Katika Ripoti ya Jumatatu, Tume imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada, Acacia ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini humo, hivyo imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.

Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni kutoka Ikulu, Rais Magufuli amemtaka waziri wa sheria Profesa Paramagamba Kabudi kupitia mikataba yote ya madini.

Ameahidi kutekeleza mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati.

Ripoti iliopita ilisababisha Waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo kusimamishwa kazi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: