BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MKUSANYIKA WA MATUKIO MANISPAA YA MOROGORO 2017

Sheikhe mkuu wa mkoa wa Morogoro, Abdallah Mkangambe akiomba dua kwa mwenyezi mungu ya kumuepushia na maadui rais Dk John Magufuli iliyofanyika uwanja wa jamhuri Morogoro, wa kwanza kushoto ni Kamanda wa polisi Morogoro, Ulrich Matei, Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini, Abdullaziz Abood na Mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT), Emmanuel Tengeneza.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris akizungumza jambo wakati wa tukio hilo la kumuombea dua rais Dk John Magufuli.


Mfanyabiashara katika soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro, Anthony Kazimoto akitayarisha magimbi kwa ajili ya kuwauzia wateja wake, magimbi, viazi vitamu, mihogo vyakula hivyo vimekuwa vikitumika kwa uwingi na waumini wa dini ya kiislama kwa ajili ya futari hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa mwezi wa ramadhani.Mkazi wa Manispaa ya Morogoro, Omari Hussein Mkwizu akisikiliza redio wakati akifuatilia matangazo ya bunge katika vikao vinavyoendelea.

Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakipinda kando ya shimo mtaa wa Makongorom eneo la CCM wilaya, shimo hilo limekuwa kero kwa watembea kwa miguu na wenye vyombo vya moto pasipo wahusika kurekebisha hali hiyo kwa kipindi kirefu.
Askari wa jeshi la polisi wakiwa wamekamata pikipiki baada ya madereva wake kuvunja sheria za usalama barabarani katikati ya mji ikiwemo kutovaa kofia ngumu.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment