BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI WA WAMILIKI WA MABASI YA ABIRIA ARUSHA

 
 

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa limetoa onyo kwa wamiliki wa mabasi ambayo yanavunja sheria za usalama barabarani. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya matokeo ya ukaguzi wa mabasi ya abiria uliofanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 22 mwezi huu hadi 24.

Kamamda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, wamiliki wa magari wanatakiwa wahakikishe mabasi yao yanazingatia ubora unaokubalika hali ambayo itasaidia abiria wanasafiri salama.

“Mbali na ubora wa gari lakini pia madereva wanatakiwa wazingatie sheria za usalama barabarani kama vile kuendesha kwa kufuata maelekezo ya alama“. Alisema Kamanda Mkumbo.

Alisema katika ukaguzi huo wa kushtukiza uliojumuisha mabasi yaliyokuwa yanakwenda mikoani na yale yaliyokuwa yanaingia jijini hapa, jumla ya mabasi 77 yalikamatwa kwa makosa ya ubovu na mwendokasi.

“Kati ya hayo mabasi 25 yalikamatwa kwa makosa ya mwendokasi ambapo 20 kati yao yalilipiwa tozo na matano wahusika walipelekwa mahakamani, wakati mabasi 52 yalikutwa na makosa ya ubovu ambapo 41 yalitozwa tozo na mabasi 11 toka makampuni mbalimbali tumeyasitishia kutoa huduma mpaka hapo yatakapofanyiwa marekebisho”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.

Kamanda Mkumbo alisema kwamba pamoja na ukaguzi wa magari hayo ambao unafanywa kila siku lakini Jeshi hilo litaendelea kufanya kaguzi za kushtukiza mara kwa mara ili kuhakikisha abiria wa mabasi hayo wanasafiri salama, huku akitoa wito kwa abiria watoe taarifa popote wanapogundua dereva anakwenda kinyume na sheria za usalama barabarani.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment