BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABAKI YA BINADAMU YA KALE YAGUNDULIWA NGOMEKONGWE TANZANIA

Utafiti unaofanywa na wataalamu wa mambo ya kale, umebaini mabaki ya binaadamu wa kale aliyezikwa katika eneo la Forodhani Ngomekongwe.

Kwa mujibu wa utafiti huo mabaki ya mtu huyo ni ameishi katika karne ya 16 na inawezekana kuwa ni wageni kutoka nchini Ureno.

Mkuu wa Divisheni na Mambo ya Kale, Abdalla Khamis Ali alisema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti hili Ofisini kwake Forodhani, akielezea utafiti huo unaoendelea katika eneo hilo.

Alisema mabaki ya mwili wa binaadamu huyo yalikutwa pembezoni mwa ukuta wa kanisa na imethibitika kuwa alikuwa ni muumini wa dini ya kikiristo.

Alisema suala la imani yake limebainika kufuatia kukutwa akiwa na msalaba, huku pia mwili wake ukiwa umezikwa miguu kuelekea mashariki na kichwa kuelekea magharibi.

Mkuu huyo alifahamisha kuwa mwili huo unakisiwa kuwa ni wa mtu mwanamke, lakini utafiti zaidi utafanyika ili kuuweza kuufanyia uchunguzi mwili huo.

Aidha alifahamisha kuwa ndani ya mabaki hayo wamebaini nembo ya kopa, hivyo kutokana na sababu tatu hizo ndizo zilizowafanya kubaini kuwa maiti hiyo ilikuwa ya kikristo.

“Maiti hii inawezekana ikawa ya mwanzo ya wareno iliyozikwa zaidi ya miaka 500 iliyopita katika eneo hilo, lakini pia inawezekana ikawa mtu huyo alikuwa kiongozi katika kanisa hilo,”alisema.

Alisema mbali ya kukuta mabaki ya mwili huo pia wamekuta mabaki ya vyombo vya kigae ambavyo vinasadikiwa kutoka nchi za nje vilivyokuwa vikitumiwa na watu waliokuwa wakiishi kipindi cha karne ya 11,12 au 13.

Hata hivyo alifahamisha kuwa utafiti huo uliofanywa kwa kutumia vitu vya kisasa walifanikiwa pia kugundua vitu vingine kadhaa vilivyokuwepo ndani ya Ngomekongwe ikiwemo kuta za majengo mbalimbali yaliyojengwa na Wareno ikiwemo kanisa na nyumba nyengine ambazo walikuwa wakizitumia kwa shughuli zao mbalimbali.Zanzibaleo
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment