BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAREKANI YATOA VITISHO VIPYA KWA KOREA KASKAZINI KUWA MUDA WA MAZUNGUMZO UMEKWISHA

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe anasema yeye pamoja na rais wa Marekani Donald Trump wamekubaliana kuwa upo umuhimu wa kupambana na Korea ya Kaskazini katika mipango yake ya majaribio ya makombora.

Abe amewaambia waandishi wa habari kuwa anashukuru kujitolea kwa Rais Trump katika suala la Korea ya Kaskazini.

Mapema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema muda wa mazungumzo umemalizika. Mapema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema muda wa mazungumzo umemalizika.

Haley amesema hakuna sababu ya kuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo hakutakuwa na matokeo, yatakayoipa mbinyo Korea Kaskazini na China ni lazima iamue kama itaamua kuchukua hatua hii muhimu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Korea kaskazini kufanya jaribio lingine la makombora yake siku ya Ijumaa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: