BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MFANYABIASHARA MKUBWA WA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA AFANYIWA UPASUAJI WA SURA ILI ASIKAMATWE NA POLISI


Polisi nchini Brazil wamemkamata mlanguzi wa madawa ya kulevya maarufu ambaye amefanyiwa upasuaji ili kukwepa kukamatwa kwa muda wa karibu miaka 30.

Luiz Carlos da Rocha ambaye pia anafahamika kama "White Head" anaaminika kuongoza genge kubwa la madawa ya kulevya barani America Kusini.

Polisi walisema kuwa hakuamu anayoweza kupewa Rocha inaweza kuwa ya karibu miaka 50 jela.

Rocha alikamatwa eno la Sorriso katika jimo la magharibu la Mato Grosson siku ya Jumamosi. Pesa na bunduki na bidhaa zinazoamika kuwa na Rocha

Amekuwa akiishi mjni humo akitumia jina Vitor Luiz de Moraes.

Polisi walilinganisha picha za zamani za Rocha na za mshukiwa ampya na kusema kuwa Luiz Carlos da Rocha na Vitor Luiz ni mtu mmoja

Polisi wa Brazil wanasema kuwa genge lake lilitambuliwa kama lenye ghasia ambalo lilikuwa likitumia maghari yasiyopenya risasi na silaha nzito.

Genge hilo lilizalisha madawa ya Cocaine nchinin Bolivia, Peru na Colombia kabla ya kusafirisha madawa hayo hadi barani Ulaya na Marekani.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment