BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWINTANGA CUP 2017 YANOGA, TIMU 15 ZATINGA 16 BORA MOROGORO

Katibu Mkuu Mtendaji chaka cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande.

Juma Mtanda, Morogoro.
Timu 15 zimefuzu kuingia hatua ya 16 bora ya mashindano ya Mwintanga Cup 2017 baada ya kufanya vizuri katika michezo yao ya hatua ya pili iliyoshirikisha timu 30 katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Katibu Mkuu Mtendaji chaka cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande alisema kuwa michezo ya hatua ya pili iliyoshirikisha timu 30 imemalizika na timu 15 zimefuzu kuingia hatua ya 16 ya mashindano ya Mwintanga Cup 2017.

Maharagande alizitaja timu zilizofuzu hatua hiyo ya 16 bora kuwani pamoja na Moro Kids, Young Star FC, Kasanga United, Black Fighter FC, Don Bocso FC, Masubo United, Ball Talent United na Chamwino Rangers.

Nyingine ni Barcelina FC ya Bigwa, Kihonda Maghorofani FC, Stend Hiace FC, Jordan Univesty, Chipopolo FC, Chicago ya Wagogo FC na Moro City FC.

Maharagande alisema kuwa michezo ya hatua ya 16 bora itaanza kutimua vumbi Julai 3 mwaka huu kati ya Young Star FC dhidi ya Kasanga United.

“Michezo ya hatua ya pili imemalizika jana (juzi) kwa timu 30 kuchuana na kupata timu 15 ambazo zimefuzu kuingia hatua ya 16 bora ya mashindano haya ya Mwintanga Cup 2017 lakini baada ya timu 15 kufuzu, timu nne zilizoshindwa hatua hiyo zitacchuana na kupata moja ili kukamilisha hatua ya timu 16.”alisema.


Maharagande. Timu zitazochuana ili kupata timu moja ya kuingia hatua ya 16 ni pamoja na Home Boys FC, Karume Rangers, Jamaica FC na JL Team FC.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment