BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATANZANIA WAMFURAHISHA RAIS MAGUFULI MWEZI JUNI 2017


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewapongeza Watanzania kwa mwamko waliounyesha wakati wa ulipaji wa kodi ya majengo.

Akizungumza leo wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Rais amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilipochukua jukumu la kukusanya kodi hiyo imewezesha wananchi kulipa kodi kwa amani.

“Walipochukua TRA, sasa waliwathaminishia kodi ambayo wananchi wanaweza kuilipa, ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi. Haijapata kutokea wananchi wakataka kulipa kodi kwa kiasi kile, ni kwa sababu ilikuwa nafuu kwao,” amesema

Pia, Rais amewataka TRA kuendelea kukusanya kodi kwa njia ambazo ni rafiki kwa kuwa wananchi hawapendi kodi inayowaumiza bali kodi ambayo ni sahihi kwao. 


“Wananchi wanapenda kulipa kodi lakini iwe na manufaa kwako,” amesema Rais Magufuli/Chanzo Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment