BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PROF LIPUMBA AZIDI KUIVURUGA CUF, AWATIMUA WABUNGE NDANI YA CHAMA

 
Kufuatia barua aliyopokea Spika wa Bunge Mhe, Job Yustino Ndugai kutoka kwa Mwenyekiti Prof, Ibrahim Haruna Lipumba na Kaimu Katibu Mkuu Mhe. Magdalena Hamisi Sakaya (Mb) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Spika angependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefukuzwa Uanachama kulingana na taratibu za Chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Wabunge hao ni: -

Mhe. Severina Silvanus Mwijage, (MB);
Mhe. Saumu Heri Sakala, (MB);
Mhe. Salma Mohamed Mwassa, (MB);
Mhe. Riziki Shahari Mngwali, (MB);
Mhe. Raisa Abdallah Mussa, (MB);
Mhe. Miza Bakari Haji, (MB);
Mhe. Hadija Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na
Mhe. Halima Ali Mohamed, (MB).

Hivyo, kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Mheshimiwa Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na pia kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa Mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo.

Imetolewa na:
Ofisi ya Spika,
S.L. P. 941,
DODOMA.
26 Julai, 2017
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: