BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 14 KWA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KUFUNGA MASHINE ZA KIELEKTONIKI HUKU VITUO 241 VIKIFUNGWA

Wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini Tanzania wamepewa siku 14 kufunga na kuanza kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti la sivyo wafutiwe leseni.

Rais Magufuli, ambaye ametoa agizo hilo, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha vituo vyote vya mafuta nchini vinatumia mashine hizo ambazo kwa Kiingereza zinafahamika kama Electronic Fiscal Petrol Printer na kusisitiza kuwa wamiliki watakaokiuka agizo hilo vituo vyao vifungwe na kufutiwa leseni.

"Na kwa hili natoa siku 14, wale wenye vituo vya mafuta wote, uwe upo Chato, uwe Biharamulo, uwe Kagera, uwe Dar es Salaam hakikisha una hiyo mashine, ndani ya siku 14," amesema Dkt Magufuli.

Mwishoni mwa wiki Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ilivifungia vituo vya mafuta kutokana kutotimiza vigezo baada ya kutofunga mashine za kielektroniki kwenye pampu za mafuta.

Kufikia Jumatatu, vituo vipatavyo 241 nchini humo vilikuwa vimefungwa na kusababisha tatizo la upatikanaji wa mafuta katika miji mingi Tanzania.

Mamlaka ya mapato ilisema wamiliki wa vituo hivyo wamekuwa wakikwepa kulipa kodi kwa kutofunga mashine hizo.

Wakati wa kuanza kutekelezwa kwa agizo hilo Jumapili, vituo 710 vilifungiwa nchi nzima lakini baadaye vituo 469 vikafunguliwa baada ya kulipia mashine hizo kwa mawakala watano walioidhinishwa kufunga mashine hizo kwa vituo vyote takribani 1800 kwa nchi nzima.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: