BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJERUMANI YATWAA KOMBE LA MABARA KWA KUITANDIKA CHILE BAO 1-0 KATIKA MCHEZO WA FAINALI NCHINI URUSI.

Timu ya taifa ya Ujerumani imetwaa taji la kombe la mabara baada ya kuishinda Chile kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Saint Petersburg nchini Urusi.

Mshambuliaji Lars Stindl ndie aliyeifungia Ujerumani goli pekee liliwapa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza baada ya kutumia vyema makosa ya kiungo wa Chile, Marcelo Diaz.

Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Ureno walifanikiwa kutwaa medali ya shaba baada ya kuichapa Mexico kwa mabao 2-1. Wachezaji wa Ureno wakishangilia.

Beki wa Ureno Luis Neto aliwapa Mexico goli la kuongoza baada ya kujifunga katika dakika ya 55, kabla ya Pepe kuzawazisha goli hilo katika dakika za lala salama.

Bao la mkwaju wa penati lilifungwa na Adrien Silva katika dakika ya 104 likawapa Ureno ushindi muhimu licha ya kumkosa nyota wake Cristiano Ronaldo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment