VIONGOZI WA CHADEMA AKIWEMO MWENYEKITI WAFUNGWA MWAKA MMOJA JELA TABORA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
VIONGOZI watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamehukumiwa kutumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko sio halali.
Viongozi hao walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Ajali Milanzi, hawakufuata sheria inayotakiwa wakati wakifanya mkusanyiko huo.
Waliohukumiwa ni Katibu Mwenezi wa Wilaya, Vincent Kananga. Wengine ni Mwenyekiti wa Tawi la Mwamsunga, Fea Rifa na Katibu wa Tawi la Mwamsunga, Luhanya Zogoma.
Awali, Mwendesha Mashtaka, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, kuwa Oktoba 30 mwaka jana kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni katika Kitongoji cha Mwamsunga walifanya mkusanyiko huo.
Alidai wakiwa wafuasi na viongozi wa chama hicho wakiwa na nia ovu, walifanya mkusanyiko usio halali kimyume cha sheria ya nchi.
Baada ya kusomewa shtaka walikana ndipo upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watatu ambao walitoa ushahidi wa kuwatambua washtakiwa.
Akitoa hukumu Hakimu Milanzi alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umewaona washtakiwa wana hatia, hivyo kila mmoja atatumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.Nipashe
0 comments:
Post a Comment