BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ULIMBOKA, JL TEAM FC WACHEMSHA NA KUSHINDWA KUTAMBA MASHINDANO YA MWINTANGA CUP 2017 MOROGORO.


Ulimboka Mwakingwe.


Juma Mtanda, Morogoro.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Ulimboka Mwakingwe ameshindwa kutamba na kikosi cha timu ya JL Team FC katika mashindano ya Mwintanga Cup 2017 baada ya kujikuta timu yake ikiambulia vipigo na kutupwa nje ya mashindano hayo Manispaa ya Morogoro.

Mwakingwe anayekinoa kikosi hicho, aliwezesha kuivusha timu hiyo kwenda hatua ya awali pili na kushindwa kukiingiza hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Katika michezo ya hatua ya pili JL Team FC ilijikuta ikitandikwa bao 5-4 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti mbele ya mahasimu wao, timu ya Kihonda Maghorofani FC kufuatia ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Katibu Mtendaji wa chama cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande alieleza kuwa timu ya JL Team FC inayonolewa na Ulimboka Mwakingwe imeshindwa kufuzu kuingia hatua ya 16 baada ya kupoteza nafasi ya hatua ya pili.

Maharagande alieleza kuwa katika michezo ya hatua ya pili, JL Team FC ilipoteza mchezo wake dhidi ya Kihonda Maghorofan FC wakikubali kupigwa bao 5-4 kwa njia ya mikwaju ya penalti baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.

“Kuna timu za JL Team FC ya Ulimboka, Mawingu United, Jamaica FC na Mawingu United zilipoteza michezo yao ya hatua ya pili ya kuingia hatua ya 16 bora lakini zikapata nafasi ya upendeleo ili mojawapo iweze kuingia katika hatua ya 16 bora.”alieleza Maharagande.

Maharagande alieleza kuwa kamati ya mashindano ya Mwintanga Cup 2017 ilizikutanisha timu hizo ili kupata timu moja ziungane na zile 15 kukamilisha idadi ya timu 16.”alieleza Maharagande.

Hatua ya pili ilikutanisha jumla ya 30 zilizopata ushindi kutoka kwenye timu 58 zilizoshiriki katika michezo ya awali ya mtoano.

Katika michezo ya hiyo timu ya Jamaica FC ilikung’utwa bao 1-0 lililofungwa na Mkude Veve dakika ya 58 na timu yake ya Mawingu kuibuka washindi huku JL Team FC ya Ulimboka Mwakingwe ikipigwa bao 4-0 na Home Boys FC katika changamoto ya mikwaju ya penalti.

Katika mchezo kati ya Mawingu United na Home Boys FC kusaka timu ya kuingia hatua ya 16 bora, Mawingu United ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Jojo Mkele dakika 56. 


Maharagande alieleza kuwa leo (jana) mchezo wa hatua ya 16 bora itaanza kwa kuzikutanisha timu za Young Star FC dhidi ya Kasanga United katika mchezo wa kufungua panzia la hatua hiyo ili kupata timu zitazoingia hatua ya nane bora ya mashindano hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: