SIMULIZI YA KUSISIMUA KUTOKA ENZI ZA UAJEMI YA KALE NA NAMNA WALIVYOKUWA WANAWATESA WATU WALIOFANYA MAKOSA
Simulizi ya kusisimua.
Wachambuzi wa Kina na Vina wa magombo ya Kale Wanajua kwa yakini kuwepo kwa Tawala kubwa NNE zilizotikisa Dunia a ya wakati huo.
1:BABYLON(Ndiyo Iraq sasa ) - chini ya Mfalme Nebuchdnezzer
2:UMEDI na UAJEMI (Ndiyo Iran kwa sasa) - Chini ya Koreshi,Altashasta na wafalme wengine baadae
3:WAYUNANI (Wagiriki) - Chini ya Alexander Mkuu.
4. DOLA LA RUMI (Italy ya Sasa) - Chini ya Kaisari.
LEO TUNAONGELEA HAWA WAAJEMI:
Hawa watu waliamini katika Haki. Na walikuwa makini sana katika kutoa adhabu zao ili mtu yoyote asionewe. Ila ukipewa adhabu kwa kosa kubwa ni adhabu hasa na usiombe ukakutana nazo.
Hapa chini ni adhabu chache.
KULAZIMISHA WATU KULA WATOTO WAO
Kama umewahi kufanya makosa madogo ya kuchukulia kawaida agizo la mkuu wa nchi, hilo ni huku sio Uajemi ya enzi hizo. Siku moja mfalme aliota ndoto mjukuu wake atampindua kwenye utawala.
Akamwagiza Jemedali wake mmoja Aitwae Harpagus amchukue huyo mjukuu na akamtupe afie Porini. Jamaa akajiongeza akamuacha huyo mtoto kwa mchunga kondoo mmoja na kulelewa hapo. Miaka kumi baadae ikajulikana kwa mfalme kuwa jamaa hakutii agizo.
Mtoto wa Harpagus alichukuliwa akakatwa mkono na kutolewa Koromeo Kisha vikarostiwa vizuri na katika sherehe iliyokuwepo jamaa akawekewa nyama ya mtoto wake. Katikati ya mlo akaulizwa kama anatambua anachokula. Ndipo mwili ulibaki ukaletwa na jamaa akalazimishwa amalizie kuula hadi atakaposhiba.
Alijua kosa lake na akaapa kuwa mtiifu na kula huyo mtoto na kuondoka na mabaki yake hadi nyumbani kwake na kumzika, Adhabu hii kwake ilitekelezwa kwa upendo na heshima nyingi.
MTU MMOJA KUUWAWA MARA TATU KWA MPIGO
Waajemi waliamini Kuna baadhi ya watu walistahili kufa zaidi ya mara moja. Ukifa haraka utakuwa umefaidi na hujajifunza.
Kiukweli Sio unakufa mara tatu ila unapitia mateso matatu makali sana kabla ya Pumzi kukata.
Towashi mmoja alipomkasirisha mke wa mfalme Cyrus. mwanamama huyo aliagiza jamaa kwanza atolewe macho yote bila ganzi. Akapewa dawa akapona baadae. Alivyopona ikaamuliwa achunwe ngozi mwili mzima. Akahudumiwa vizuri hadi aliopata nafuu ndio wakammalizia kwa kumsulubisha hadi kifo.
Hiyo sio mara moja. Siku nyingine wakiwa vitani mwanajeshi mmoja alipomuona mfalme amejeruhiwa akataka kumuua bila mafanikio. Mama wa mfalme akaagiza wamuache yeye mwenyewe atamshughulikia.
Kwanza alimfunga kwenye matairi mawili akavutwa pande zote nusu kugawanyika vipande viwili halafu akaachwa hivyohivyo siku kumi. Baadae mama huyo akamtoa macho yote mawili.
Baada ya hapo alichukua Uji wa chuma unaotokota (kama umezoea maji 100C hapo ni zaidi ya 1000C) akaumimina masikioni hadi jamaa akafa kifo hicho cha tatu, Hawa ndio wamama wa kiajemi enzi hizo.
KULIWA NA WADUDU HADI KUFA
Unaweza kudhani hii ni adhabu nyepesi sana.
Hapa ilikuwa hivi, Yule mtu ambaye alikuwa amechukiwa na mfalme.
Mtesi maalumu alichaguliwa. Mteswaji anaingizwa kwenye gome la mti kama hapo juu linalomtosha na kuzibwa chini akiwa amesimama na sehemu ya mwili wake uko njee.
Anaanza kunyweshwa asali na maziwa taratibu hadi atakapoa za kuarisha na gogo zima kujaa kinyesi. Akiwa katika hali hiyo anaachwa kidogo atulie.
Kisha Anapakwa asali sehemu ya mwili inayoonekana na wadudu, nyuki, dondora wanaanza kumtembelea na kumng'ata hadi anafikia pointi ya kutaka kufa.
Hapo anaanza kulishwa tena kidogo kidogo ili asife mapema huku akiendelea kung'atwa na wadudu wakiingia masikioni na mapuani.
Zoezi hili lilichukua takribani siku 17 kabla ya mteswaji kupoteza fahamu na maombi yake ya muda mrefu ya kufa kujibiwa.
Silimulizi kutoka kwa Geofrey Chambua, anapatikana katika ukurasa wake wa facebook kwa kubofya hii link hapa chini.
https://www.facebook.com/profile.php?id=100008895961948
0 comments:
Post a Comment