BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALOKOLE WASABABISHA VIFO VYA WAUMINI WAWILI WAKATI WAKIWABATIZA KATIKA KINA KIREFU CHA MAJI KATIKA MTO UNGWASI


WAUMINI wawili wa Kanisa la Pool of Siloam Ministry wilayani Rombo wamekufa maji baada ya kuzama kwenye kina kirefu wakati wakibatizwa katika Mto Ungwasi.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa waumini hao waliopoteza maisha wakiwa kwenye ibada ya ubatizo, wakiwa ni miongoni mwa watu wazima 30 waliokuwa wameandaliwa kubatizwa kabla ya zoezi hilo kuvurugika.

“Waliokufa walisababisha zoezi hilo lisiendelee tena na hivyo hao wengine waliokuwa nao wabatizwe wakanusurika ila Polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo,” alisema Hokororo.

Habari zaidi zilieleza kuwa kabla ya vifo hivyo kutokea, ibada ilikuwa imeanza majira ya saa 6:00 na mkasa huo ukatokea saa 8:00 mchana wa juzi kwenye Mto Ungwasi ambao upo katika kata za Ushiri-Ikueni na Mrao Keryo.

Kwa mujibu wa Hokororo, tayari Jeshi la Polisi limemtia nguvuni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo aliyekuwa akiendesha ibada hiyo ya ubatizo pamoja na watuhumiwa wengine wawili.

Alisema miili ya waumini hao iliopolewa na kisha kupelekwa Hospitali Teule ya Huruma kwa ajili ya kuhifadhiwa na kusubiri taratibu nyingine za uchunguzi wa kitabibu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Hamisi Issah alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alithibitisha waumini hao kufa maji, lakini akasema atatoa taarifa rasmi baada ya kutoka kwenye ukaguzi wa miradi Wilaya ya Hai.

Nipashe ilimtafuta Diwani wa Kata ya Ushiri-Ikueni, Bernard Ngowi ili kujua undani wa tukio hilo ambaye alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

”Hapo walipofia hao waumini wawili wa kanisa la Siloam ni mpaka unaotenganisha Kata za Mrao Keryo na Ushiri-Ikueni," alisema Ngowi na kwamba "mmoja wa waliokufa ambaye anaitwa Utowu anatokea Kata ya Makiidi."

"Huyo mwingine hatujafahamu jina lake lakini ni wa Kata ya Keni Aleni.” Tukio jingine kama hilo lilitokea Desemba 19, mwaka 2016 katika eneo la Mailisita, Wilaya ya Hai ambako muumini wa kanisa moja la kikristo, Issa Juma alikufa maji, muda mfupi baada ya kubadili dini yake ya awali na kubatizwa katika Mto Mailisita.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: