BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAOHOJI SERIKALI KUZUIA UUZAJI WA CHAKULA NJE YA NCHI YA TANZANIA NI WASHAMBA TU

Mbunifu wa mtambo wa kukatia magugumaji, Emmanuel Bukuku akiwasha mashine hiyo katika banda la Veta, ikiwa ni siku ya pili ya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam juzi. Picha na Anthony Siame

Dar es Salaam. Uchumi wa viwanda unaenda sambamba na kuzuia kuuzwa mazao holela, imeelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema wanaohoji hatua ya Serikali kuzuia kuuzwa mahindi, machungwa na mazao mbalimbali nje ya nchi ni ushamba kwa sababu uchumi wa viwanda unahitaji malighafi zikiwamo za mazao.

Alisema agizo la kuzuia kusafirisha mazao si jipya na wakati huu litakuwa na msisitizo zaidi kwa sababu kila kitu kitafanyika katika viwanda vya ndani na kusafirisha nje vikiwa tayari kwa kuliwa badala ya kupeleka kwa ajili ya kusindikwa.

Mwijage akizungumzia maonyesho ya Sabasaba, alisema yatatumika kama kipimo kwa wajasiriamali wadogo na kuwakutanisha na sekta muhimu ikiwamo wakulima katika kufikia uchumi wa viwanda.

Alisema muda wa kuuza malighafi nje ya nchi na kurudi kuuziwa juisi au pumba ni ushamba usiokubalika.

Waziri alisema hatua iliyopo ni kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinakuwa na thamani.

Alisema Serikali inaendeleza juhudi kuhakikisha hakuna mazao yanayosafirishwa nje ya nchi yakasindikwe huko halafu yarudi kama bidhaa. “Tunataka kama ni muhogo, mahindi, ngano, kunde, mbaazi iondoke ikiwa imetayarishwa badala ya kwenda ghafi,” alisema Mwijage.

Waziri huyo alisema ujenzi wa kiwanda kikubwa cha matunda wilayani Korogwe utaongeza chachu ya kuhamasisha wawekezaji nchini.

Mwijage aliitaka jamii kutambua jitihada za Serikali katika kuhamasisha uwekezaji kwenye mazao jamii ya kunde ili kuongeza thamani. Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage alisema Rais John Magufuli ameagiza uzinduzi wa maonyesho hayo leo ufanyike saa nne asubuhi badala ya saa nane mchana ili apate muda wa kukutana na wajasiriamali wadogo. 


Alisema Rais ataonana na wajasiriamali wadogo banda kwa banda ili kusikia wanachokifanya na changamoto wanazokabiliana nazo.

Mwijage alisema mbali ya kukutana na wafanyabiashara wadogo, atakutana pia na wakubwa pia.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: