BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

COSAFA YATOA ZAWADI YA DOLA 10,000 KWA TAIFA STARS BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA TATU AFRIKA YA KUSINI

Baraza la Mpira wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa Taifa Stars ya Tanzania baada ya kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.

Fedha hizo ni sawa na Sh. 22,000,000 ambako Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeamua fedha hizo kwa mgawanyo sawa, zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na benchi la ufundi.

Kadhalika Cosafa limetuma fedha za zawadi kwa wachezaji wa Tanzania ambao walifanya vema kwenye mchezo mmoja baada ya mwingine katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvutio wa aina yake kwa mafanikio ya timu ya Tanzania.

Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi; Muzamiru Yassin aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola; Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed alyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili. Tanzania iliifunga Lesotho na kushika nafasi ya tatu.

Wakati huo huo bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.

Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’.

Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:-

Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.

Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro.

Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

……………………………………………………………..………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: