BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Kiungo wa zamani wa Yanga SC, Haruna Niyonzima kufichuliwa rasmi Simba Day

Hatimaye Simba imethibitisha kumalizana na kiungo Haruna Niyonzima na atatua nchini mwishoni mwa wiki kujiunga na timu tayari kwa Tamasha la Simba Day.

Usajili wa Haruna Simba ulikuwa na usiri mwingi na kuwaacha mashabiki wengi katika maswali, wengine wakiamini mchezaji hiyo kasajiliwa kweli na wengine wakiwa na mashaka kuwa ni uongo.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wameshakamilisha usajili wa Niyonzima baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika na atajiunga na timu mwishoni mwa wiki.

"Hatuna haja ya kuficha hivi sasa. Kweli Niyonzima ni mchezaji wetu tumeshamalizana naye na atajiunga na timu mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

"Hajajiunga na kambi ya Afrika Kusini kwa sababu aliutaarifu uongozi kuwa kuna mambo anashughulikia hivyo hadi kufikia Jumamosi atakuwa amefika," alisema Manara.

Aliongeza, "Anaweza kuja na ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda ambayo timu itakuja nayo Jumamosi, hivyo wanaweza kumpitia au yeye mwenyewe anaweza kutangulia.

Niyonzima aliichezea Yanga kwa misimu mitano na mpaka sasa mashabiki wa klabu hiyo hawaamini kama kweli kiungo huyo fundi ameitosa klabu hiyo na kwenda kwa wapinzani wao.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment