BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MANUEL NORIEGA, RAIS DIKTETA ALIYETAWALA NCHI YA PANAMA
Na Geofrey Chambua 
Manuel Antonio Noriega Moreno alikua mwanasiasa na mwanajeshi wa nchi ya Panama pia infoma/mdaku wa Shirika la Kijasusi la Marekani (C.I.A) wa kipindi kirefu. Alikua mtawala wa kijeshi wa Nchio ya Panama na dikteta tangu mwaka 1983 mpaka 1989 wamarekani walipovamia nchi hiyo kijeshi na kumuondoa madarakani.

Alizaliwa jijini Panama na kusoma katika moja ya shule za kijeshi mjini lima na baada ya hapo ya sekondari ya Americans. 


Baada ya hapo alijiunga na jeshi la Nchi hiyo na kuwa mmoja wa maafisa wa jeshi,alifanya kazi kwa karibu na mkuu wa intelijensia wa jeshi la nchi hiyo na kupanda vyeo ambapo baada ya Omar Torrijo ambaye ndiye aliyekua mkuu wa intelijensia wa jeshi kufanya jaribio la mapinduzi na kushinda alipewa nafasi hiyo mwaka 1968.

Norriega alikua moja ya vyanzo muhimu vya kuamnika vya C.I.A. kwenye masuala ya intelijensia, pia ilikua ndio sehemu muhimu ya kuanzishia, kupanga pamoja na kupitishia silaha na fedha linapokuja suala la operasheni yoyote inayohusu masuala ya kijeshi marekani ya kati na kusini.

Norriega pia alijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya hasa cocane kwa kiwango cha hali ya juu kitu ambacho wamarekani walikifahamu fika kwa miaka mingi, ila waliliruhusu suala hilo liendelee kwa sababu za umuhimu wa Norriega kwenye masuala ya kijeshi na kiusalama katika ukanda huo wa marekani ya kati na kusini.


Utawala wa Norriega katika Nchi hiyo uligubikwa na ukandamizwaji wa vyombo vya habari, uimarishwaji wa jeshi, pamoja na uteswaji na ukandamizwaji wa mahasimu wa kisiasa. Noriega aliweza kusimamia uchaguzi wowote na kupata matokeo anayotaka yeye, alijitengenezea utajiri mkubwa kupitia biashara yake ya madawa ya kulevya.

Taratibu mahusiano yake na Nchi ya marekani yalianza kupungua kwa sababu ya vitendo hivyo pamoja na kuanza kuuza taarifa za kiintelijensia kwa mahasimu wa marekani. Mwaka 1988 Norriega alibainishwa kwamba ni mmoja wa watu wanaosafirisha madawa ya kulevya katika miji ya Miami Florida. 


Marekani waliiivamia Panama 1989 na kumuondoa madarakani na kumpeleka marekani kama mfungwa wa kivita ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 40japo baadae kilipunguzwa hadi miaka 30 jela.

Kifungo cha Norriega nchini marekani kilisitishwa mwaka 2007 baada ya Nchi ya Panama pamoja na Ufaransa kuomba kumuhukumu bila yeye mwenyewe kuwapo mahakamani (Ex parte) kwa mauaji mwaka 1995 na utakatishaji wa fedha mwaka 1999. 


Ufaransa ilikabidhiwa mtuhumiwa huyu mwaka 2010 mwezi wa nne baada ya ombi lao kukubaliwa na alifikishwa Paris 27|4|2010 na baada ya kesi yake kusikilizwa upya alihukumiwa kifungo cha miaka saba, mwezi wa saba 2010.

Makubaliano ya kumhamisha gereza kutoka Ufaransa na kumpeleka Panama kutumikia kifungo cha miaka 20 yalifikiwa ikiwa ni vifungo vyote vilivyomkabili nchini marekani pamoja na ufaransa hivyo alipelekwa panama 23|09|2011. 


Norriega alifariki katika hospitali ya Santo Thomas katika jiji la Panama 29|05|2017 miezi miwili baada ya uperation ya ubongo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment