Hata kabla ya matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais nchini Kenya kutangazwa Ijumaa tarehe 11 Agosti, muungano wa upinzani nchini humo ulikuwa umechukua msimamo usiokuwa wa kawaida - kwamba hautawasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo hayo licha ya kutoyakubali.Hilo lilishangaza kwani katika mataifa ya kidemokrasia, mahakama huwa ndiyo taasisi iliyo na jukumu la kuhakikisha haki inatendeka iwapo raia au taasisi yoyote itajihisi kutotendewa haki.
Aidha, ndiyo njia pekee iliyosalia sasa ambayo inaweza kumpa tena Bw Raila Odinga matumaini ya kuingia madarakani au kujaribu tena kuingia madarakani iwapo itabatilisha ushindi wa Bw Kenyatta.
Muungano huo ulikuwa siku moja baada ya uchaguzi kufanyika, umeandaa kikao na habari na kutangaza kwamba walikuwa wamegundua mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa.
Walidai wadukuzi walikuwa watu wenye uhusiano na serikali ya Jubilee na kwamba waliingilia na kuchakachua matokeo kumfaa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa akishindana na Bw Raila Odinga kwa mara ya pili.
Kuhusu tuhuma hizo za udukuzi, walipotakiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu ni nani hasa aliyehusika, pamoja na jinsi walivyopata nyaraka za taarifa kuhusu sava matukio katika sava moja ya tume hiyo, walikataa kata kata.
Tume ya uchaguzi ilisema mwanzoni ilikuwa haina taarifa kuhusu udukuzi kama huo lakini kwamba ingelifanya uchunguzi. Saa chache baadaye, tume hiyo ilisema hakuna jaribio lolote la udukuzi lililokuwa limefanyia katika sava ya matokeo ya uchaguzi.
Waliofuatilia kisa hiki, walitarajia kwamba huu ungekuwa msingi wa muungano wa upinzani National Super Alliance katika kupinga matokeo ya urais kortini.
La pili lilikuwa tuhuma kuhusu sajili ya wapiga kura, ambapo kabla ya uchaguzi kufanyika, muungano huo ulikuwa umedai tume ilikiuka sheria katika kuchapisha orodha rasmi ya wapiga kura vituoni ndipo wananchi waihakiki na kuhakikisha kuna uwazi.
Baadhi ya wanachama wa NASA walidai kuna watu waliokuwa wamefariki ambao walikuwa bado kwenye sajili hiyo, na wengine ambao hawakuwa wametimiza umri wa kupiga kura ambao walikuwa na vitambulisho na walikuwa kwenye sajili. Tume ya uchaguzi ilikanusha tuhuma zote.
Naibu ajenti mkuu wa Nasa, seneta James Orengo alisema saa chache kabla ya matokeo kutangazwa: "Kwenda kortini si njia ambayo tutatumia, tumekuwa huko awali. Si njia ambayo tutatumia… Kila wakati uchaguzi ukiibiwa, Wakenya wamesimama na kuhakikisha mabadiliko yanafanyika kuimarisha nchi."
"Hakuna anayefaa kufikiri kwamba huu ndio mwisho. Hakuna anayefaa kutufanya tujihisi kuwa na hatia, kwani tuna njia nyingine za kikatiba za kuchukua kupinga mambo yaliyofanywa na tume."
Kwa kusema hivyo, alionekana kugusia njia ya kuwaita wananchi kushiriki maandamano au mgomo kushinikiza mageuzi.
Wachanganuzi wamekuwa wakifuatilia msimamo wa Nasa na yanayojitokeza ni mambo mawili makuu ambayo huenda yanaufanya muungano huo kutoamini kwamba utashinda iwapo utawasilisha kesi kortini.
1. Ushahidi
Kuna uwezekano kwamba huenda muungano huu haujapata ushahidi wa kutosha wa kuhakikisha wanaweza kuwasilisha kesi yenye uzito mahakamani na kushinda. Kwa hilo, huenda hawataki kujiingiza katika mbio ambazo wanajua tayari watakuwa wameshindwa.

0 comments:
Post a Comment