BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHERIA YA MADINI KUANZA KUNG'ATA HUKU NA KULE, YAWABANA WEZI

SHERIA ya Madini ya mwaka 2010 imefanyiwa mabadiliko makubwa, hivyo kuanzia sasa mambo ya utoaji wa Leseni za Madini umesimamishwa hadi itakapoundwa Tume au Kamisheni ya Madini kama sheria inavyotaka.

Sheria ya Madini imefanyiwa mabadiliko makubwa na mabadiliko ya Sheria 2017 (Sheria Iliyoandikishwa na Mengineyo ya Mwaka 2017 ( Written Law Miscellaneous Ammenfments 2017), iliyopitishwa na kikao cha Bajeti na imesheheni makatazo ya mambo mengi ili kubana utoroshaji wa mapato ya Serikali.

Sheria hiyo imefuta Wakala wa Madini iliyojulikana kama Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) na ofisi nane za kushughulikia madini nchini.

Kwa maelezo ya Profesa James Mdoe, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, amewaambia waandishi wa habari kuwa wale wanaotaka kupeleka madini nje wanatakiwa kulipa ‘Clearing Fee’ ya kiwango cha asilimia moja ya thamani ya madini hayo, ambayo yamefanyiwa ukaguzi na kuthaminishwa na Ofisi ya Kamishina wa Madini kwa muda huo wa mpito hadi Kamisheni ya Madini itakapoanza kazi rasmi baada ya kuundwa.

Aliainisha kuwa, hayo ni pamoja na majukumu yote ya kazi iliyokuwa inafanywa na TMAA kwa muda itafanywa na ofisi hiyo, ikiwamo makusanyo ya mrabaha kwa madini ya ujenzi na ya viwanda, uthibitishaji wa vocha za malipo na usalama wa madini migodini.

Majukumu mengine yaliyoathirika ni usimamizi wa migodi kwa kupitia mahitaji ya wazalishaji wote wa madini na miradi yao, ukaguzi katika sehemu za kutokea na kusafirisha mizigo, ikiwamo viwanja vya ndege na mipaka ya nchi pamoja na bandari kuzuia upoteaji madini kwenda nje.

Profesa Mdoe alisema kuwa, mrabaha kuhusu madini mbalimbali umeongezeka, ambapo madini ya metali kama dhahabu, shaba na fedha yameongezeka kutoka kiwango cha awali cha asilimia 4 hadi asilimia 6. Wakati huohuo madini ya vito na ya thamani kama almasi, yakuti, ganeti na tanzanite yameongezeka mrabaha kuwa wa asilimia 6 kutoka za awali asilimia 5.

Wachimbaji wadogo kulipa kodi
Alisema sheria mpya inataka kila mtu au taasisi katika mnyororo wa thamani atailipa serikali kwa mapato na huduma mbalimbali ambapo tozo ya asilimia 5 kwa mara ya kwanza itakusanywa na madalali na wafanyabiashara wakubwa (dealers) kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo kama kodi ya makusanyo (withholding tax) na kuwasilishwa kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA)

Amewataka wadau wote kushirikiana na wafanyakazi waliopo, kwani wanafanya majukumu yao kama ilivyoainishwa na Wizara na katika misingi ya sheria kwa mafanikio makubwa kukusanya maduhuli yote ya serikali katika wakati huu wa mpito.

Aliwahakikishia wafanyakazi ambao hawakuhusika na mtafaruku wa biashara ya madini kuwa wataendelea na kazi kama kawaida na kupata stahiki zao za malipo kwa mpangilio mpya hadi hapo mabadiliko yatakapofanyika kikamilifu kwa sheria mpya.

Wafanyakazi hao wameambiwa wataendelea kutoa mwendelezo wa leseni za wachimbaji wadogo wadogo, kwa vile maofisa wote wa TMAA na wale wa ofisi za kanda wako chini ya kanda, wakati utambulisho na vifaa vya kazi vyote vitatolewa na Kamishina wa Madini, vikiwamo mihuri, lakiri na risiti, vikionesha ofisi hiyo ya Kamishina wa Madini.

Mabadiliko haya ni matokeo ya ripoti mbili zilizoanzishwa na Rais John Magufuli kuchunguza kuhusu mwenendo wa biashara ya madini na makinikia, ambayo ilifichua uozo na wizi wa kutisha na udanganyifu uliokithiri wa rasilimali za taifa za madini zenye thamani ya mamia ya shilingi trilioni na hivyo Bunge kubadilisha sheria mbalimbali zilizoleta mabadiliko makubwa ambayo yamelenga uboreshaji huduma na ukusanyaji mapato ya taifa.

Matokeo yake kwa undani ni kupata sheria tatu ambazo zina mtazamo wa kuboresha Uchumi wa nchi, zikiwamo (Written Laws Miscellaneous Act , 2017, Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act 2017 na Natural Wealth and Contracts Review and Renegotiation of Unconscionable Terms Act 2017.

Sheria hizo wanadai wengi ni sawa na tangazo la vita kwa ubeberu, mtazamo ambao Rais Magufuli ameuona na Waziri wake wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuukubali.Mtanzania
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: