BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SUPER MAHAKAMA FC YATOA VITISHO MASHINDANO YA RWAKATARE UCP 2017 KILOMBERO


Kocha wa timu ya soka ya Super Mahakama FC ya Mngeta wilaya ya Kilombero, Gaudence Massati akitoa maelekezo wakati wa mchezo kati yao na mahasimu wao Mchombe Ranger FC katika mashindano ya Rwakatare Cup 2017 yanayoendelea kwenye uwanja wa shule ya msingi Lukolongo.

Juma Mtanda.

Na Juma Mtanda, Morogoro
Timu ya soka ya Super Mahakama FC ya Mngeta imefichua siri ya kushiriki mashindano ya Rwakatare Cup 2017 kuwa inatumia mashindano hayo kama njia ya maandalizi kwa ajili ya ligi ya mkoa wa Morogoro kwa lengo la kukusanya nguvu ya kutwaa ubingwa wa mkoa huo ili kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa wa mikoa ngazi ya taifa.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Kocha mkuu wa Super Mahakama FC, Gaudence Massati alisema kuwa tayari wamekufuzu na kuingia hatua ya pili baada ya kuisambaratisha Black Power FC kwa bao 3-0 katika mchezo wao wa awali.

Michezo hiyo inashirikisha jumla ya timu 80 zilizogawanywa kwenye vituo saba vya Mngeta, Mlimba, Mkamba, Ifakara, Chita, Namawala na Mang’ula ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha zawadi ya sh2 milioni huku wa pili akimbulia sh1 milioni.

Massati alisema kuwa mashindano hayo anayatumia kuangalia mapungufu na kuandaa kikosi imara kuelekea ligi daraja la tatu ngazi ya taifa mkoa wa Morogoro na kuwania nafasi ya kuwa bingwa wa mkoa huo.

“Super Mahakama FC ipo ligi daraja la tatu na lengo la kuingia Rwakatare Cup 2017 ni kujiweka fiti kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya mkoa wetu na tumeweka dhamira ya kubwa bingwa wa mkoa wa Morogoro msimu huu.”alisema Massati.

Massati alisema kuwa dhamira yao ni kuona wanacheza ligi ya mabingwa wa mikoa ili kusaka tiketi ya kuingia ligi daraja la pili kisha daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu Tanzania bara kwani wana vijana wenye vipaji vya kucheza soka la kufundishwa.

Mratibu wa vituo cha Mngeta, Supa Duma alitaja timu nane zilizofuzu baada ya kupata ushindi katika michezo ya awakuli ni pamoja na Machinga FC ilipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Ijia FC, Mchombe Rangers FC ikaizaba Kidete FC bao 5-4 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Nyingine ni Black Mamba FC ikatandikwa bao 2-1 na Mija FC, City Boys ikipata ushindi wa bao 3-0 kwa Home Sport Club, Muungano FC ilisambaratishwa na Mbasa FC kwa bao 8-7 kwa penalti kufuatia sare ya bao 3-3.

“Baada ya hatua ya awali kumalizika kwa kushirikisha timu 16, timu nane zilizoingia zitacheza ligi ili kupata timu mbili zitakazoungana na timu za vituo saba kuelekea kusaka bingwa wa Rwakatare Cup 2017.

Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro, Tanuwili Bahanuzi alisema kuwa ligi hiyo kwa sasa inachezwa katika vituo vinne kikiwemo cha Mngeta, Mlimba, Mkamba na Chita huku vituo vingine vikiwa katika maandalizi ya mwisho ya kuanza ligi hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: