Mbunge wa kuteuliwa CCM mkoa wa Morogoro, Mchungaji Dk Getruda Rwakatare akipiga mpira na kufunga bao kwa njia ya mkwaju wa penalti kama ishara ya mashindano ya Rwakatare Cup 2017 yanayoshirikisha jumla ya timu za soka 80 ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa sh2mil na mshindi wa pili sh1mil yaliyozzinduliwa katika kijiji cha Mng'eta uwanja wa Lukolonga wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro.Na Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya soka ya Super Mahakama FC imeendeleza wimbi la ubabe mashindano ya Rwakatare Cup 2017 kituo cha Mngeta kufuatia kuifumua kwa kuikandamiza Muungano FC kwa kuitandika bao 7-0 wakati wa michezo ya kusaka nafasi ya kutinga nusu fainali ya mashindano hayo yanayochezwa katika vituo saba katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Msimamizi wa kituo cha Mngeta, Supertus Duma alisema kuwa Super Mahakama FC imekuwa ya kwanza kutinga nusu fainali katika kituo baada ya kushinda michezo mitatu dhidi ya Mchombe Rangers FC iliyokung’utwa bao 2-0, Stone Fire FC ikachalazwa bao 3-0 na Muungano FC yenyewe ikatandika bao 7-0.
Duma aliwataja wachezaji waliopelekea huzuni kwa timu ya Muungano FC kuwa ni, Ally Lyungu alifungua panzia ya kalamu ya magoli kwa kufunga bao la kwanza dakika ya tano, John Nyanyali akifunga la pili dakika ya nane, Isaya Nyanyali akipachika bao la tatu dakika ya 22.
Mabao mengine yalipachikwa na, Bob Said aliyefunga mabao mawili dakika ya 36 na 66 huku Damas Lukowa naye akifunga mawilia dakika ya 70 na 78 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Lukolongo Mngeta na Super Mahakama FC kuibuka na ushindi mnono wa bao 7-0.
Duma alisema kuwa timu nyingine zilizotinga nusu fainali kituo cha Mngeta ni pamoja na Mngeta Rangers FC, Stone Fire FC na City Boys FC ambapo michezo ya nusu fainali itachezwa Agosti 17 mwaka huu kusaka timu mbili zitakazounga na timu nyingine za vituo saba kuunda ligi ya timu 14 kusaka bingwa wa Rwakatare Cup 2017.
Katika kituo cha Mlimba, timu za Teachers FC na Street FC zenyewe tayari zimefuzu baada ya kumalizika kwa michezo ya kituo hicho na kupata timu mbili zitakazo kwenda Mngeta kuungana na timu nyingine za vituo sita kuunda timu 14 zitakazoingia kwenye kinyang'anyiro cha fainali kusaka bingwa.
Kwenye michezo ya nusu fainali timu ya Teachers FC iliiondosha Miwangani FC kwa bao 3-0 huku Street FC ikiisambaratisha Mlimba City FC kwa penalti 4-3 baada ya sare ya bao 3-3 katika michezo yao ya nusu fainali.alisema msimamizi wa kituo cha Mlimba, Ditrum Mhenga.
Kwa upande wa kituo cha Mkamba, timu nane zenyewe zimetinga robo fainali ya mashindano hayo baada ya kufanya vizuri katika michezo ya makundi.
Msimamizi wa kituo hicho, Clarence Msavila alizitaja timu zilizofuzu robo fainali ni pamoja na Mkamba Rangers FC, Kidatu FC, CDA FC, Mwendokasi FC, Serenegeti Boys FC, TP Mazembe FC,Chicago FC na Maquapa FC.
Katika kituo cha Namawala wenyewe walianza kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Komoa FC iliyopokea kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Mofu FC iliyopata mabao kupitia kwa mshambuliaji wake, Sunday Mganga aliyeifungia timu yake mabao yote mawili.

0 comments:
Post a Comment