BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAGENI WAFURIKA KATIKA KIJIJI CHA CHONGOLEANI MKOANI TANGA

WAKATI Rais John Magufuli na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, leo wanaweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi hapa Tanga, Tanzania, maandalizi yote ya uzinduzi wa mradi huo wa kihistoria yamekamilika, humu mji ukifurika na kupeleka neema kwa wafanyabiashara wa nyumba za wageni, vyombo vya usafiri na kadhalika.

HabariLeo jana lilitembelea Chongoleani na kukuta wahusika wakikamilisha ujenzi wa jukwaa, upangaji viti na uwekaji wa mahema. Juzi katika eneo hilo hilo, gazeti hili pia ilishuhudia wazee wa eneo mitaa ya Putini na Chongoleani wakiomba dua ili shughuli ya leo na zitakazoendelea kufanyika katika eneo hilo zipate baraka za Mwenyezi Mungu.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na Meya wa Mji wa Tanga, Seleboss Mustafa, wamewataka wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia uwekaji huo wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba hilo linalotazamiwa kuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: