BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYEFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI, SERIKALI YAMTETEA BAADA YA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MIWILI KILOMERO

Licha ya kukiri kosa la kumbaka mtoto wa miaka miwili na miezi mitano na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, Simon Mwakalinga amerejea uraiani baada ya mahakama kumwachia huru kutokana na Serikali kumtetea.

Mwakalinga alihukumiwa adhabu hiyo na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mwaka 2007 baada ya kukiri kutenda kosa hilo, Septemba 23, 2007 Kijiji cha Mlabani, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani imemfutia adhabu hiyo huku akiwa ameshatumikia takribani miaka 10, baada ya kukata rufaa na Serikali ikamuunga mkono kupinga adhabu yake.

Kutoka na kukiri kwake kosa, Mahakama ya Wilaya ilimtia hatiani na kumhukumu kifungo cha maisha jela, lakini baadaye alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambayo katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Aisha Nyerere Novemba 18, 2009, ilitupilia mbali rufaa yake na kukubaliana na hukumu ya mahakama ya wilaya.

Mwakalinga alikata rufaa Mahakama ya Rufani, ambayo iliungwa mkono na Serikali. Katika rufaa yake, Mwakalinga alitoa sababu nne za rufaa lakini ni mbili zilizoonekana kuwa za msingi.

Sababu hizo mbili ni kauli yake ya kukiri kosa ambayo ilitumiwa na Mahakama kumtia hatiani na kuungwa mkono na Mahakama Kuu, ilikuwa kauleni, yaani mtu asiyetumainiwa.

Pia, alikuwa akidai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa na kasoro kisheria.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa yake hiyo iliyosikilizwa na jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Mbarouk Mbarouk, Richard Mziray na Sivangilwa Mwangesi, Mwakalinga alijiwakilisha mwenyewe kwa kuwa hakuwa na wakili wa kumwakilisha.

Wakili wa Serikali, Clara Charwe akisaidiana na mwenzake, Lilian Rwetabura aliieleza mahakama kuwa wanamuunga mkono mrufani na kwamba hawakubaliani na hukumu na adhabu aliyopewa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: